Mtu anayedaiwa kuwa muuaji wa mfululizo nchini Zimbabwe ameshtakiwa kwa tuhuma za mauaji.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Thedolwenkosi Ndlove mwenye umri wa miaka 2o alikuwa anawawinda wahasiriwa wasio na makazi na baada ya kuwaua alisemekana kula matumbo yao katika mauaji ya siku nane katika mji mkuu wa Harare.
Thadolwenkosi Ndlovu, amehusishwa na kukithiri kwa mauaji matano yaliyotokea kote jijini kati ya Agosti 28 na Septemba 4, alipokamatwa na polisi wa Zimbabwe, vyombo vya habari viliripoti.
Bw. Ndlovu anaripotiwa kuwaua waathiriwa wake kwa kuwaangusha zege vichwani walipokuwa wamelala kabla ya kutoa viungo vyao kwa kutumia vioo vilivyovunjika.
Akiwa amefikishwa kortini Harare siku ya Jumatano, Bw. Ndlovu alionekana kurudi nyuma akikiri kwamba alipika na kula nyama ya wahasiriwa wake.
Alidai kuwa ungamo la ulaji nyama lilitolewa kwa kushinikizwa na wapelelezi.
Anadaiwa kukata na kuchoma matumbo ya waathiriwa kwenye moto wazi kabla ya kuwateketeza.
Polisi walisema kuwa Bw. Ndlovu pia alikuwa akitaka kukata sehemu za siri za mmoja wa waathiriwa wake, lakini alitoroka eneo la tukio kabla hajafanikisha hilo.
Bw. Ndlovu, ambaye anaripotiwa kukosa makao mwenyewe, amewekwa rumande.
Bw. Ndlovu anashtakiwa kwa makosa matano ya mauaji na mawili ya kujaribu kuua.
Pia inafahamika kuwa hapo awali alikaa gerezani huko Harare na Bulawayo, mji alikozaliwa. Pia anaripotiwa kuhusishwa na kesi tatu za mauaji huko Bulawayo, kusini-magharibi mwa Zimbabwe, mwaka 2020, The Herald ya nchini humo iliripoti.
Kulikuwa na hofu kubwa miongoni mwa watu machokoraa mjini Harare huku habari za mauaji ya Bw. Ndlovu zikienea, Ripoti zinaonyesha kuwa baadhi walikuwa wameanza kulala katika vikundi kwa ajili ya usalama wao au walikuwa wameondoka kwa muda mjini Harare.
‘Tuliamua kuhama jiji tukihofia maisha yetu’, mwanamume mmoja asiye na makao aliambia The Herald.
‘Nina bahati ya kuwa hai, naweza kuwa nimekufa kwa sasa. Hebu wazia kuchomwa moto kwa kustarehesha,’ Panashe Uchena, 16, aliambia The Standard ya nchini humo.
'Amekamatwa, lakini bado nina hofu. Mitaani si salama tena.'