• Jambo la kushukuru ni kwamba uingiliaji kati wa haraka wa mwendesha mashtaka na afisa wa kibali wa mahakama uliokoa hakimu.
Drama ilizuka katika mahakama moja mjini Accra, nchini Ghana baada ya mfanyibiashara mmoja aliyekuwa ameshtakiwa kukabidhiwa kifungo cha miaka 15 jela.
Kwa mujibu wa Ghana News Agency, mwanamume huyo aliyetambulika kama Frank Kwesi Obeng alibaini kwamba amekabidhiwa kifungo cha miaka 15 jela.
Hapo ndipo alicharuka kwa hasira kama za Mkizi na kuvua shati yake huku akimtoa mbio jaji aliyempa hukumu huo kwa lengo la kumpiga.
Mara tu baada ya hakimu kutoa hukumu hiyo, mfanyibiashara huyo aliuliza: “Tafadhali unanifahamu mahali fulani, kwa nini umenipa kifungo cha miaka 15 jela?”. Kisha akakimbia kuelekea kwa hakimu, Bi Evelyn Asamoah, iliripotiwa.
Jambo la kushukuru ni kwamba uingiliaji kati wa haraka wa mwendesha mashtaka na afisa wa kibali wa mahakama uliokoa hakimu na kupelekwa haraka chumbani kwake salama huku Obeng akiongozwa kifua wazi na bila viatu vyake kutoka mahakamani.
Inafurahisha, mke wa Obeng na mshtakiwa mwenzake, Joyce Safowaa, pia walikuwa kizimbani na alipatikana na hatia ya njama ya kuiba, kuficha uhalifu na kuiba GH712, 229 [shilingi 9,128,000za Kenya] kutoka kwa Mavis Toffan, mlalamishi.
Sawasawa na mumewe, Safowaa alipoarifiwa kwamba lazima afungwe jela miaka 10. Alipiga kelele, "Mungu, ninaota!" huku akilia na kukaa kwenye kiti huku akionekana kutokuamini.
Ripoti zinasema wafuasi wengi waliomiminika katika mahakama hiyo pia walipinga uamuzi huo, wakielezea mashaka yao kuhusu madai ya mlalamishi.