Video: Mamia ya wahitimu wa NYS wafurika Embakasi Barracks wakitaka kazi ya KDF

Baadhi wanahisi kwamba Wakenya wengi wanazidi kufinywa na gharama ya juu ya maisha hivyo kuliweka kuwa suala la kufa kupona wanaposikia nafasi za kazi zimetangazwa. Nafasi zilizotangazwa ni 350 tu!

Muhtasari

• Katika tangazo la wiki jana, KDF ilibainisha kuwa waombaji kazi wanaostahiki wanapaswa kuwa na barua ya idhini kutoka NYS.

Mamia ya watu waliotaka kazi ya KDF.
Mamia ya watu waliotaka kazi ya KDF.
Image: Screengrab

Video imeibuka mitandaoni ikionesha mamia ya watu waliotajwa kuwa ni wahitimu wa huduma ya vijana kwa taifa, NYS wakiwa wanang’ang’ania nafasi chache zilizotangazwa na jeshi la Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa, jeshi la Kenya KDF lilikuwa limetangaza nafasi 350 pekee za kuchukuliwa kwa wahitimu wa NYS katika jeshi hilo lakini cha ajabu ni kwamba mamia walifurika na kukanyagana kila mmoja ambaye aliwahi maliza kozi ya NYS alikuwa anajaribu bahati yake.

Katika tangazo la wiki jana, KDF ilibainisha kuwa waombaji kazi wanaostahiki wanapaswa kuwa na barua ya idhini kutoka NYS na wawe wamepata alama ya chini ya daraja D katika Cheti cha Elimu ya Sekondari ya Kenya (KCSE).

Uajiri huo unakuja ikiwa ni wiki moja baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwaajiri makurutu maalum wa KDF pamoja na wafanyabiashara na wanawake ambayo ilifungwa Ijumaa, Septemba 8.

Jumla ya watahiniwa 1,606 wamo katika kinyang’anyiro cha kujiunga na kikosi hicho, 347 kati yao walifuzu nafasi za maofisa wataalamu huku 1,259 wakitafuta nafasi ya wafanyabiashara na wanawake.

Katika video hiyo inayoonyesha kila mmoja kutoka NYS akijaribu kujipatia nafasi ya kuwa wa kwanza langoni Embakasi Garisson Barracks, imezua maoni kinzani mtandaoni.

Baadhi wanahisi kwamba Wakenya wengi wanazidi kufinywa na gharama ya juu ya maisha hivyo kuliweka kuwa suala la kufa kupona wanaposikia nafasi za kazi zimetangazwa.

 

 

Baada ya uandikishaji wa waajiriwa wa NYS kukamilika, kikosi kitaanza mahojiano ya walioteuliwa kuanzia Jumatatu wiki inayofuata.

Tazama video ya mng'ang'ano huo hapa chini;