Piga magoti mbele ya Raila, omba msamaha - Eric Omondi amshauri Jalang'o

“Ninachopenda kumshauri Jalang’o ni kwamba, aamke mapema, ajiandae, ale kifungua kinywa, aingie kwenye gari lake na kuelekea kwa Baba Raila Amollo Odinga, apige magoti mbele yake na kuomba msamaha,” alisema.

Muhtasari

• Alipoulizwa iwapo atawania kiti cha Lang'ata iwapo Jalang'o atatimuliwa, alisema sauti ya watu ni sauti ya Mungu.

• Alisema hataki hali ya mbunge huyo kuachia kiti cha Lang’ata kwa kuwa atakuwa amemwangusha.

Eric Omondi na Jalang'o
Eric Omondi na Jalang'o
Image: Screenshot

Mcheshi Eric Omondi amemshauri Mbunge wa Langáta Phelix Odiwuor almaarufu Jalangó kwenda kumwomba msamaha kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga.

Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio mnamo Ijumaa, Omondi aliambia Jalang'o pia kuomba msamaha kwa wakazi wa Lang'ata, chama cha ODM na Mungu.

“Ninachopenda kumshauri Jalang’o ni kwamba, aamke mapema, ajiandae, ale kifungua kinywa, aingie kwenye gari lake na kuelekea kwa Baba Raila Amollo Odinga, apige magoti mbele yake na kuomba msamaha,” alisema.

"Baada ya hapo, anafaa kurejea bungeni, kuomba msamaha kutoka kwa wapiga kura na kisha kuelekea kanisani ili aombe msamaha kwa Mungu pamoja na wanachama wa ODM."

Omondi alisema ikiwa Jalang'o hataenda mbele ya wale anaopaswa kuwaomba msamaha, basi asahau kuhusu kufanikiwa.

Alipoulizwa iwapo atawania kiti cha Lang'ata iwapo Jalang'o atatimuliwa, alisema sauti ya watu ni sauti ya Mungu.

Alisema hataki hali ya mbunge huyo kuachia kiti cha Lang’ata kwa kuwa atakuwa amemwangusha.

"Tatizo langu kubwa kwa sasa sio Lang'ata bali ni Rais William Ruto. Kwa kawaida huwa nawaambia watu kwamba kuhusu lang'ata, sauti ya watu ni sauti ya Mungu. Sauti zote nimekuwa nikisikia kuhusu mimi kuwania nafasi hiyo." kiti si sauti yangu bali ni ya Mungu