Kizaazaa kanisani fundi wa majeneza akimsihi pasta kuombea biashara yake kushamiri

Mchungaji aliita kila mtu mwenye hitaji maalum kujongea kwenye madhabahu ili kumwambia hitaji ambalo angependa kuombewa kwa Mungu.

Muhtasari

• Mwanamume huyo seremala alijongea kwa unyenyekevu mbele ya madhabau akiwa tayari na ombi lake.

• "Amekwenda kanisani akamwambia pasta naomba uombee biashara yangu istawi kwa sababu biashara imedidimia sana,” sehemu ya ujumbe huo ilisomwa na mtangazaji.

Jeneza tupu.
Jeneza tupu.
Image: Maktaba

Muumini wa kanisa moja humu nchini amewashangaza wasikilizaji wa kituo kimoja cha redio humu nchini baada ya kuhadithia tukio lililotokea katika kanisa anakoabudu.

Kwa mujibu wa ujumbe huo ambao ulisomwa hewani asubuhi ya Jumatatu Septemba 25, jamaa huyo ambaye ni fundi seremala wa kutengeneza majeneza alikwenda kanisani kwa ibada ya Jumapili kama kawaida.

Baada ya mahubiri, mchungaji aliwaita waumini weney uhitaji maalum kujongea kwenye madhabahu wakiwa na ombi ambalo wangependa mchungaji awafikishie kwa Mungu.

Mwanamume huyo seremala alijongea kwa unyenyekevu mbele ya madhabau akiwa tayari na ombi lake.

“Amekwenda kanisani akamwambia pasta naomba uombee biashara yangu istawi kwa sababu biashara imedidimia sana,” sehemu ya ujumbe huo ilisomwa na mtangazaji.

Mchungaji alijitolea kumuombea lakini mwanzo akamuuliza ni biashara gani ili kwamba aweke mambo sawa wakati anatuma ombi hilo kwa Mungu kulijibu.

Mtumishi wa Mungu alipigwa na butwaa baada ya fundi seremala kutamka waziwazi kwamba alikuwa anataka biashara yake ya kutengeneza na kuuza majeneza iombewe ili inawiri, kwa kile alisema kwamba katika siku za hivi karibuni imekuwa ikididimia kwa kukosa wateja – wafu.

“Wateja hawaji na sipati kipato cha kukimu mahitaji yangu kama iluivyokuwa hapo awali. Naomba uniweke kwa maombi biashara iinuke tena. Biashara yangu ni fundi wa majeneza,” alisema huku mchungaji akishtuka na kusita huku umati uliokuwa unaguna ukisita kwa kimya cha ghafla.

Watangazaji walichagiza katika ujumbe huo mmoja akijaribu kuiga jinsi mchungaji angeombea biashara ya muumini wa kanisa lake ili kupata faidia na baadae kurudisha shukrani ya fungu la kumi kwa Mungu baada ya biashara kushamiri.