Mume wangu alimuoa mwanangu bila yangu kujua-Mwanadada asimulia kwa uchungu

Wakati wa sasa na karne hii inaonekana kutoheshimu ndoa au kuwa na heshima ya baba na mtoto.

Muhtasari
  • Kulingana na mwanamke huyo, miaka imepita kama mwanawe anamkataza kuingia kwenye chumba chake cha kulala, kwani alidai alihitaji faragha yake.
Mwanamke mwenye huzuni
Mwanamke mwenye huzuni
Image: HISANI

Ni mambo ambayo tumekuwa tukiyaona kwanye filamu na kusema au kufikiria kwamba hayawezi kutupata.

Wakati wa sasa na karne hii inaonekana kutoheshimu ndoa au kuwa na heshima ya baba na mtoto.

Mengi yamewatokea wanandoa huku wengi wakiwachwa na kovu moyoni mwao.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii mwanamke mmoja amewaacha wanamitandao midomo wazi baada ya kusimulia jinsi alivyogundua mwanawe ambaye ni kifungua mimba wake alikuwa mke wa pili wa mumewe.

Kulingana na mwanamke huyo, miaka imepita kama mwanawe anamkataza kuingia kwenye chumba chake cha kulala, kwani alidai alihitaji faragha yake.

Mwanamke huyo alisema kwamba mwanawe alibeba ujauzito hivi karibuni na walifurahi sana na mumewe kwani walitaka na kutamani sana kukua na wajukuu.

"Mume wangu alinioa nikiwa na mtoto wa kike ambaye alichukua jukumu la kumlea na wakakuwa karibu sana, niliona upendo wa baba na mwana kati yao wala hamna kitu ambacho nilifikiria kibaya

Mtoto wangu alikuwa akikuwa mgonjwa mume wangu alikuwa anamshughulikia ipasavyo,miaka imepita na wala sijawahi ingia kwenye chumba cha mwanangu tangu afikishe miaka 18,mwaka mmoja uliopita mwanangu alipata ujauzito. na tulifurahi sana kwamba tulikuwa tunatarajia mjukuu

Aliweza kujifungua na mtoto wa kike,hivi majuzi aliikuwa mgonjwa na kwa ajili ni kazi ya baba yake kumshughulikia, hakuwa karibu, na tangu alihitaji kula na mwanawe nilienda kwenye chumba chake  amabcho amekuwa akifunga muda wote,nilipata picha za hafla yake ya harusi na mume wangu, na wala hawajawahi niambia wala kuonyesha dalili zozote sijui nifanye nini,"Alisimulia mwanamke huyo.

Je ingekuwa ni wewe ungefanya nini kuhusu suala hilo?