Video: Muuza mitumba asimulia kurudi nyumbani na kuambiwa alizikwa Julai

Jamaa huyo alisema kwamba mwili wa mtu anayedhaniwa kuwa ni yeye alipata umezikwa kando ya kaburi la baba yake na kuwa yeye ndiye mvulana mkubwa katika familia yake.

Muhtasari

• Hapo ndipo alikutana na ukweli mchungu kwa kuambiwa kwamba yeye ni mzimu kwani Ochieng mwenyewe walishamzika kitambo mnamo mwezi Julai.

alphonse ochieng,
alphonse ochieng,
Image: Screengrab

Jamaa mmoja mfanyibiashara wa nguo za mitumba kutoka kaunti ya Nakuru amewashangaza wengi baada ya kuahdithi jinsi alivyotaarifiwa kwamba alizikwa miezi mitatu iliyopita hali ya kuwa yuko hai.

Alphonse Okoth Ochieng, mkazi wa Nakuru katika mahojiano na Nation alisema kwamba kilichofanya familia yake kuhisi pengine amefariki ni baada ya kubadilisha mazingira ya biashara kutoka Nakuru kwenda Nairobi.

Baada ya kufanya biashara hiyo katika soko kubwa tambarare la Gikomba, aliamua kununua laini ya simu na kupigia familia yake kuwajulia hali.

Hapo ndipo alikutana na ukweli mchungu kwa kuambiwa kwamba yeye ni mzimu kwani Ochieng mwenyewe walishamzika kitambo mnamo mwezi Julai.

“Nilikosana na mke hapa Nakuru nikaona badala ya kumfanya kitu kibaya acha nibadilishe mazingira kidogo. Nikaondoka kwenda Nairobi bila simu bila kitu chochote. Wiki tatu zilizopita nikanunua simu Ngara na laini, nikapiga simu kuuliza huyu mke wangu wanaendelea namna gani, akaniambia hapana, wewe tulikuzika Julai, nilishtuka sana,” Ochieng aliambia Nation.

Jamaa huyo alisema kwamba mwili wa mtu anayedhaniwa kuwa ni yeye alipata umezikwa kando ya kaburi la baba yake na kuwa yeye ndiye mvulana mkubwa katika familia yake.

Alitoa wito kwa mamlaka kufanya ihnsani kufukuwa mwili ule ili kuuondoa katika boma lao kwani yeye kuiona pale na kuambiwa kuwa ni yake ni jambo linalomuumiza roho sana.

“Ningeweza kusikia vizuri sana ili niweze kuwa na Amani, ule mwili utolewe pale na kurudishwa hadi hapa Nakuru. Hata watu weneywe walishtuka, kwa sasa hata watu wakinikuta wengine wanaanza kukimbia, wengine wanaanza kuniambia mazishi yangu walichanga pesa niwarudishie,” alisema kwa simanzi.

Ochieng alisema kwamba kwa sasa hajaamini kwamba aliweza kuzikwa akiwa hai na shughuli zake nyingi zimesimama kwani hawezi enda nyumbani kwao wala kukutana na watu wa kwao mpaka pale mila na matambiko ya jamii ya Luo yatakapofanyika ili kumrudisha tena kwenye jamii kujumuika na wenzake.