Mtoto afa maji kwenye bwawa nyumbani wazazi wakiwa bize kuvuta bangi

Polisi pia waligundua kuwa nyumba nzima ilikuwa na "harufu kali ya bangi iliyovutwa" walipokuwa wakitazama huku na kule kumtafuta mvulana huyo.

Muhtasari

• Ortiz na Ruiz waliambia polisi kuwa wana kadi za matibabu zilizotolewa na serikali na walisema wanaivuta bangi "mara kwa mara."

• Angalau ilikuwa mara ya nne kwa mtoto kuondoka kwenye makazi peke yake, ripoti Zaidi zilisema.

Smoking
Image: The Star

Wazazi wawili wametiwa mbaroni nchini Marekani katika jimbo la Florida kufuatia kisa cha kustaajabisha ambapo inaarifiwa walimtelekeza mwanawe hadi kufa maji kweney bwawa la kuogelea nyumbani huku wakiwa bize kuvuta bangi chumbani.

Kwa mujibu wa NYP, polisi walibaini kuwa mtoto huyo anaugua tawahudi na alikwenda kweney bwawa la kuogelea kabla ya kuzama na kufa kwa kile kilisemekana kwamba ni utepetevu wa wazazi ambao kipindi hicho chote walikuwa wanavuta bangi.

Angalau ilikuwa mara ya nne kwa mtoto kuondoka kwenye makazi peke yake, ripoti Zaidi zilisema.

Polisi walisema wazazi wa mvulana huyo, Barbara Ruiz na Lester Ortiz, walikuwa na macho ya damu na walikuwa wakinuka "bangi freshi" wakati maafisa walipofika baada ya Ortiz kuripoti kwamba mtoto wao alitoweka dakika 30 kabla.

Wazazi wote wawili wanakabiliwa na mashtaka ya kuua bila kukusudia.

Polisi pia waligundua kuwa nyumba nzima ilikuwa na "harufu kali ya bangi iliyovutwa" walipokuwa wakitazama huku na kule kumtafuta mvulana huyo, Ethan Ortiz Ruiz, 3, ambaye mwili wake ulipatikana ukielea kwenye kidimbwi moja kwa moja nyuma ya nyumba yao kama dakika 20 baadaye.

Alipelekwa katika Hospitali ya Lake Monroe huko Sanford kwenye jimbo hilo, ambako alitangazwa kuwa amefariki.

Kulingana na polisi, Ethan alikuwa ameondoka kwenye nyumba hiyo bila wazazi wake kujua angalau mara nyingine tatu.

Mara mbili kati ya hizo, aliletwa kwenye ofisi ya mbele na majirani wenye msaada ambao walimwona kijana huyo akitembea kuzunguka jumba la ghorofa bila kusimamiwa.

Katika hafla ya tatu mnamo Machi, mjumbe wa wafanyikazi wa usimamizi wa jumba la ghorofa aliwaita polisi baada ya kumwona Ethan kwa mara nyingine tena nje peke yake.

Ortiz aliwaambia maafisa kuwa alikuwa amelala bila kujua mvulana huyo alikuwa ameondoka.

Polisi walisema wakati wa ziara hii kwenye ghorofa hiyo kwamba waliona mvulana huyo aliweza kufungua mlango wa mbele peke yake, licha ya hatua za ziada za usalama ambazo zilikuwa zimewekwa kumzuia kufanya hivyo.

Ortiz na Ruiz waliambia polisi kuwa wana kadi za matibabu zilizotolewa na serikali na walisema wanaivuta bangi "mara kwa mara."