logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kiambu: Padri wa kanisa Katoliki afunga ndoa baada ya kuasi kanuni za ukuhani

Aliporudi Kenya, aliamua kuoa katika sherehe ya kitamaduni. Wenzi hao walijaliwa watoto wawili.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri23 October 2023 - 03:49

Muhtasari


• "Nina furaha sana. Kwa mke wangu, naahidi kukupenda siku zote,” alisema.

Mwanamke aliyekuwa anajifungua apoteza mtoto baada ya sista kukataa kutoa ambulensi kumkimbiza hospitalini.

Waumini wa kanisa katoliki katika eneo la Githunguri kaunti ya Kiambu Jumapili walishuhudia harusi ya kipekee ambayo wengi hawajawahi kuishuhudia katika maisha yao.

Harusi hiyo ya kipekee ilikuwa ya padre muasi wa kanisa katoliki ambaye alimuoa mke wake miaka kadhaa baada ya kuasi kanuni za kanisa hilo kwamba padr hafai kuoa.

Kasisi Edwin Gathang’i Waiguru Jumapili alifunga ndoa ya kupendeza na Margaret Wanjira Githui katika bustani ya Michael’s Pot huko Ikinu Githunguri.

Harusi hiyo ilihudhuriwa na mamia ya familia na marafiki wa wanandoa. Padre huyo alitawazwa kuwa kasisi wa Kikatoliki siku hiyohiyo.

Padre Waiguru alisema baada ya kutumwa kuhubiri Amerika Kaskazini na Kusini, alihisi haja ya kuoa na kuwa na familia.

Aliporudi Kenya, aliamua kuoa katika sherehe ya kitamaduni. Wenzi hao walijaliwa watoto wawili.

Alitawazwa tena kama kuhani wa Karismatiki na pia akafunga ndoa yake. Alisema sasa anaweza kusema ameishi kwa wito wake wa ukuhani.

"Nina furaha sana. Kwa mke wangu, naahidi kukupenda siku zote,” alisema.

Sherehe ya kutawazwa iliongozwa na Askofu Patrick Mulau wa kanisa la Kirinyaga Charismatic ambaye alisema kanisa lake ni la Roma katoliki pekee lakini linatofautiana tu kuhusu sakramenti ya Ndoa ambapo makasisi wa Kanisa lake huoa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved