logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamke ashinda kesi ya kufidiwa Sh451m baada ya kuchomwa na chai aliyopewa hotelini

Majeraha ya mwanamke huyo yalisababisha zaidi ya $200,000 [milioni 30 za Kenya].

image
na Davis Ojiambo

Habari26 October 2023 - 13:59

Muhtasari


  • • Majeraha ya mwanamke huyo yalisababisha zaidi ya $200,000 [milioni 30 za Kenya] katika bili za matibabu, Welch alisema.
  • • Kesi hiyo inadai kuwa ajali hiyo haingetokea ikiwa mfanyakazi wa mgahawa angeweka kifuniko vizuri kwenye kikombe cha kahawa.
Kikombe cha Chai moto

Mwanamke mmoja wa jimbo la Georgia nchini Marekani ametunukiwa dola milioni 3[ sawa na shilingi milioni 451 za Kenya] katika utatuzi wa kesi baada ya kudaiwa kuchomwa vibaya na kikombe cha kahawa alichopewa kwenye mgahawa mmoja.

Kwa mujibu wa toleo la NYP, Wakili wa wa mwanamke huyo mweney umri wa miaka 70 alisema katika taarifa kwamba mwanamke huyo alilazimika kujifunza tena jinsi ya kutembea na bado anahangaika na shughuli za kila siku, baada ya kuhudumiwa kikombe cha moto cha kahawa mnamo Februari 2021.

"Amerika inaweza kukimbia kwenye Dunkin, lakini mteja wetu alilazimika kujifunza tena jinsi ya kutembea kutokana na ukali wa majeraha yake," wakili Welch alinukuliwa.

"Majeraha ya kuchomwa kwake yalikuwa makali sana hivi kwamba alikaa kwa wiki katika kitengo cha kuungua huko Grady Health na imebidi abadilishe kabisa maisha yake. Kutembea bado kunamletea uchungu, hawezi kwenda nje kwenye jua, na lazima apake mafuta na marashi kwenye majeraha yake ya kuungua mara kadhaa kwa siku.”

Kulingana na Welch, mwanamke huyo alienda eneo la Sugar Hill, Georgia, mgahawa wa Dunkin na kuagiza kikombe cha kahawa moto.

Baada ya mfanyakazi huyo kumpa kahawa hiyo, kifuniko cha kikombe cha kahawa kilimtoka, kikimwagikia kahawa, na kusababisha majeraha ya moto ya daraja la pili na la tatu kwenye mapaja, kinena, na tumbo.

Majeraha ya mwanamke huyo yalisababisha zaidi ya $200,000 [milioni 30 za Kenya] katika bili za matibabu, Welch alisema.

Kesi hiyo inadai kuwa ajali hiyo haingetokea ikiwa mfanyakazi wa mgahawa angeweka kifuniko vizuri kwenye kikombe cha kahawa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved