Nandi: Chifu ajitoa uhai baada ya kumfumania mkewe akifanya mapenzi na polisi

Douglas Chikanda, Afisa wa Upelelezi wa Jinai wa Kaunti ya Nandi, alithibitisha tukio hilo, linalohusisha mmoja wa maafisa wake na mke wa chifu.

Muhtasari

• Tukio hilo lilitokea wakati afisa wa polisi, wa kituo cha  Kobujoi, alipomtembelea mke wa chifu katika vyumba vya kulala vya kukodisha eneo la Sereme, Kaunti ya Nand. Chifu alipofika alisikitika sana kumkuta mkewe na afisa wa polisi wakifanya kitendo kisicho halali.

Kitanzi
Kitanzi
Image: HISANI

Katika kisa cha kusikitisha kilichotokea Jumatatu katika eneo la Ndurio, Kaunti ya Nandi, chifu mwenye umri wa miaka 42alijitia kitanzi baada ya kumfumania mkewe akifanya tendo la ndoa na afisa wa polisi

Douglas Chikanda, Afisa wa Upelelezi wa Jinai wa Kaunti ya Nandi, alithibitisha tukio hilo, na kulitaja kamasuala la kimapenzi  linalohusisha mmoja wa maafisa wake na mke wa chifu.

Tukio hilo lilitokea wakati afisa wa polisi, wa kituo cha  Kobujoi, alipomtembelea mke wa chifu katika vyumba vya kulala vya kukodisha eneo la Sereme, Kaunti ya Nand. Chifu alipofika alisikitika sana kumkuta mkewe na afisa wa polisi wakifanya kitendo kisicho halali.

Akiwa amezidiwa na mshtuko na kukata tamaa, chifu huyo alikunywa dawa ya kuua wadudu, ya ‘Round Up,’ kama ilivyofichuliwa na mwanafamilia aliyezungumza na polisi.

Alikimbizwa haraka katika hospitali ya White Crescent kwa matibabu ya haraka,ila juhudi hizo zikagonga mwamba na kufariki kwa kuzidiwa na dawa hiyo.

Mwili wake ulihamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya White Crescent, ambako unasubiri uchunguzi wa maiti.

Wakati huo huo, wapelelezi katika Kaunti ya Nandi wameanzisha uchunguzi ili kubaini habari kamili kuhusu hali hii ya kusikitisha.

Katika kukabiliana na tukio hili , afisa wa polisi aliyehusika amepewa likizo ya lazima, akisubiri uchunguzi wa kina wa suala hilo.

Tukio hili sio tu kwamba linaashiria janga la kibinafsi lakini pia linatoa mwanga juu ya kuongezeka kwa kutisha kwa visa vya ukosefu wa uaminifu ndani ya ndoa. Data ya hivi majuzi kutoka Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) , ilionyesha kwamba wanaume Wakenya, kwa wastani, wana wapenzi saba katika ndoa.