logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanafunzi wa Pwani University waomboleza kifo cha mwenzao kwa kuwasha mishumaa

Faith Adongo,aliripotiwa kufariki kutokana na shambulio ambapo alidungwa visu.

image
na

Habari31 October 2023 - 05:24

Muhtasari


• Hafla hiyo ilipangwa na kikundi cha undugu wa wanafunzi huku yake yakitarajiwa kufanyika baadaye nyumbani kwao Homa Bay.

 


Faith Adongo

Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Pwani, waliandaa hafla ya kuomboleza kifo cha mwanafunzi mwenzao Faith Adongo aliyeuawa Oktoba 20 kwa kuasha  mishumaa kwa heshima yake.

Hafla hiyo ilipangwa na kikundi cha undugu wa wanafunzi huku yake yakitarajiwa kufanyika baadaye nyumbani kwao Homa Bay.

Diana Wanjiru,ambaye ni kiongozi wa wanafunzi,aliwalika  wanafunzi wenzake kwa minajili ya kuchangisha kusaidia katika gharama ya mazishi.

"Kwa hivyo,nitowe wito kwa wanafunzi wote kwa ajili ya hafla kubwa ya kuchangisha fedha na kuwasha mishumaa kwa ajili ya kumbukumbu ya mwenzetu. Sote tujitokeze kwa shehima ya mwenzetu,"alisema.

Picha za hafla hiyo zilionyesha wanafunzi hao wakiungana na kuwasha mishumaa huku wakifanya maombi na kuimba nyimbo za kufariji.

Hata hivyo, wanafunzi hao walitoa wito kuwepo kwa haki kwa mwenzao,na kuomba serikali kuimarisha usalama katika maeneo hayo.

Faith Adongo,aliripotiwa kufariki baada ya kuvamiwa na kudungwa  kisu usiku wa Oktaba 20,alipokuwa akirejea  nyumbani.

Alikimbizwa katika hospitali ya kaunti ya kilifi,ila kwa bahati mbaya akaaga dunia kwa kuvuja damu nyingi.

Vifo vya wanafunzi hasa wa vyuo vimeshuhudiwa mfululizo kwa  katika muda wa hivi punde.

Katika tukio tofauti,mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Daystar,naye aliaga dunia kwa njia tatanishi,ambapo uchunguzi unaendelea kubaini kifo hicho.

Kifo cha Mercy Cherono,pia kilijiri siku chache baada ya kusajiliwa katika chuo hicho,ambapo walikuwa wamehudhuria tamasha la wanafunzi wapya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved