Jinsi Mfalme Charles alivyowafurahisha wengi kwa Kiswahili sanifu katika ikulu

“Mabibi na mabwana, hamjambo? Niaje? Ni furaha yangu kubwa kuwa na nyinyi jioni ya leo…” mfalme Charles alisema kwa sehemu.

Muhtasari

• “Mabibi na mabwana, hamjambo? Niaje? Ni furaha yangu kubwa kuwa na nyinyi jioni ya leo…” mfalme Charles alisema kwa sehemu.

King Charles
King Charles
Image: Facebook//William Ruto.

Lugha ya Kiswaili ni moja ya lugha pendwa na zenye umaarufu Zaidi duniani.

Hili lilidhihirika Jumanne katika ikulu ya Nairobi wakati wa ziara ya mflame Charles wa tatu kutoka Uingereza.

Mfalme huyo akiandamana na mkewe Malkia Camilla na viongozi mbalimbali wa Kenya katika dhifa iliyoandaliwa katik ikulu ya Nairobi na mwenyeji wake Rais Ruto, aliwafurahisha wengi katika hotuba yake alipoamua kuzungumza Kiswahili.

Katika hotuba yake, mfalme alitaka kujichanganya na wasikilizaji wake; aliongea maneno machache ya Kiswahili japo kwa lafudhi yake kali ya kigeni, akiwaacha wasikilizaji katika vicheko. Katika hotuba yake, mfalme alistaajabu kupata fursa ya kurejea Kenya baada ya miaka mingi.

“Mabibi na mabwana, hamjambo? Niaje? Ni furaha yangu kubwa kuwa na nyinyi jioni ya leo…” mfalme Charles alisema kwa sehemu kabla ya kupigiwa makofi na kuendeleza hotuba yake kwa lugha yake ya nyumbani – Kiingereza.

Alitangulia kumsifu rais kwa mapokezi mazuri aliyopewa yeye na mkewe katika siku ya kwanza ya ziara yao ya kifalme barani Afrika. Mfalme huyo alijivunia kwa Kenya kuwa nchi yake ya kwanza kuzuru tangu kutawazwa kwake mwaka jana.

Pia alijutia madhira ambayo wapiganiaji uhuru wa Kenya walipitia mikononi mwa wakoloni wa taifa lake kati ya mwaka 1952 hadi 1960.

"Ni furaha kubwa kwa mke wangu na mimi kurejea Kenya kwa mara nyingine. Ninamshukuru sana rais kwa mwaliko wa ukarimu zaidi kwa ziara hii ya kiserikali; ukarimu mkubwa ambao mmetuonyesha na makaribisho mazuri ajabu,watu wa Kenya wametupokea. Imenigusa sana," alisema.