Ajuza wa miaka 76 afunga ndoa na ng'ombe aliyempa kiss kama ya marehemu mume wake

Mume wa mjane huyo alifariki mwaka jana na alipoonja ulimi wa ng'ombe huyo, alihisi kabisa aina ya busu la ng'ombe lilifanana na la mume wake na hivyo kufanya uamuzi wa kuoana na ng'ombe

Muhtasari

• Khim Hang, 76, anayeishi katika jimbo la Kratie la Kambodia, alishangazwa na ufanano kati ya ng'ombe huyo na mwenzi wake aliyekufa.

Mjane afunga ndoa na ng'ombe
Mjane afunga ndoa na ng'ombe
Image: Hisani

Unaambiwa kila sekunde iendayo kwa Mungu katika ulimwengu huu, maajabu hayakawii kutokea.

Nchini Kambodia mjane wa miaka 76 ameafikia uamuzi wa kufunga ndoa na ng’ombe ambaye alimbusu na kuibua kumbukumbu za busu la marehemu mumewe, The Sun wanaripoti.

Khim Hang, 76, anayeishi katika jimbo la Kratie la Kambodia, alishangazwa na ufanano kati ya ng'ombe huyo na mwenzi wake aliyekufa.

Mara ya kwanza alipokutana na mnyama huyo, Bi Hang alisema alilamba nywele na shingo yake, akambusu, kisha akamfuata ghorofani.

Ilikuwa ni kile ambacho mume wake - ambaye alikufa mwaka uliopita - angeweza kufanya na akasadiki kuwa alikuwa akikutana na kuzaliwa kwake tena.

Bi Hang aliliambia shirika la habari la Reuters:

"Ninaamini kwamba ndama huyo ni mume wangu kwa sababu chochote anachofanya... ni sawa na jinsi mume wangu alivyofanya alipokuwa hai."

Wanandoa wasiotarajiwa walioana muda mfupi baadaye, kulingana na majirani.

Picha za ajabu zilionyesha mwanamke huyo akiongoza ng'ombe hadi kwenye nyumba yake ya orofa kabla ya kuoga na kumuandalia kitanda - akiwa na mito iliyotumiwa na marehemu mumewe Tol Khut.

Mtoto wa Bi Hang alisema "aliweza kuhisi roho ya baba yake ndani ya mnyama" na alihakikisha kwamba hatembei mbali sana na nyumba yao.

Mwanamke huyo amewakataza watoto wake kuuza au kumdhulumu ng’ombe huyo baada ya kufa, na kuwaamuru badala yake wamchunge “baba” yao hadi mnyama huyo atakapofariki dunia.

Hata katika kifo, anataka waitende kwa heshima ambayo wangefanya kama mwanadamu na kufanya mazishi ya kitamaduni.