Nyoka wa mrembo mcheza filamu za watu wazima auma uume wa mteja wakiwa chumbani (video)

“Nataka kuwatambulisha kwa Betty. Yeye ni chatu wangu….Ana urefu wa futi 8 hivi. Sijawahi kuwa na tatizo na kuumwa kwake au kitu chochote hadi leo,” mrembo huyo mwenye umbo zuri alikiri kwenye.

Muhtasari

• Baada ya kutoka kuoga, Dabello alimweka nyoka kwenye shingo ya rafiki yake asiyejua, na kuelekea bafuni kuoga.

• Alianza kuondoka chumbani lakini ghafla alishtushwa na "mayowe" yake makubwa.

Mrembo na nyoka wake wa kufugwa.
Mrembo na nyoka wake wa kufugwa.
Image: Instagram

Nyota wa filamu za watu wazima kutoka Australia anayeitwa Dani Dabello katika mtandao wa Instagram amewafungukia wafuasi wake baada ya tukio la kutisha la hivi majuzi ambapo nyoka-kipenzi wake mkubwa alimvamia mpenzi wa kiume katika eneo la faragha walipokuwa wakifanya mambo yao.

Alieleza simulizi hiyo ya kustaajabisha kwenye chapisho la hivi majuzi kwenye Instagram akisema kwamba ‘ni wakati wa simulizi na nyoka wangu kipenzi’.

“Nataka kuwatambulisha kwa Betty. Yeye ni chatu wangu….Ana urefu wa futi 8 hivi. Sijawahi kuwa na tatizo na kuumwa kwake au kitu chochote hadi leo,” mrembo huyo mwenye umbo zuri alikiri kwenye video ya Instagram iliyochapishwa Jumatano, inayoonyesha nyoka huyo akiwa amejifunga shingoni mwake.

Dabello na rafiki yake walikuwa wametoka tu kurekodi maudhui ya faragha pamoja, wakati mambo yaliripotiwa kubadilika ghafla kutoka kuwa ya kuvutia hadi ya kutisha.

"Kwa hivyo hapo awali nilikuwa na rafiki yangu na tukapiga video ... mara tulipomaliza kufanya hivyo aliruka kuoga, lakini alisema alitaka kushikilia nyoka wangu kipenzi baadaye," mwigizaji huyo alifichua.

Baada ya kutoka kuoga, Dabello alimweka nyoka kwenye shingo ya rafiki yake asiyejua, na kuelekea bafuni kuoga.

Alianza kuondoka chumbani lakini ghafla alishtushwa na "mayowe" yake makubwa.

‘Niligeuka na kuona kwamba Betty ameshikilia [sehemu zake nyeti] na amejaribu kumtoa,” alisema. ‘

"Baada ya dakika chache tulimtoa na nikamrudisha ndani ya boma lake na kulikuwa na damu kila mahali hivyo tukasafisha yote hayo," aliongeza.

Baada ya kumng'oa nyoka huyo kwenye uume wake, alikagua ili kuhakikisha kuwa "hakuna meno madogo yaliyosalia ndani yake" kwa sababu chatu wakati mwingine huacha meno yao ndani ya vitu baada ya kuwauma.

Hii si mara ya kwanza kwa matukio kama haya ya ajabu yanaripotiwa haswa katika mataifa ambayo ufugaji wa nyoka ni jambo la kawaida.

Itakumbukwa mwaka 2021, toleo la New York Post liliwahi ripoti kwamba mwanamume Mholanzi mwenye umri wa miaka 47 alilazimika kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha uume wake baada ya cobra kumuuma uume wakati wa safari ya ziara nchini Afrika Kusini - na kusababisha kuoza.

Mnamo 2020, kijana wa Thai alilazwa hospitalini baada ya nyoka kuuma uume wao huku kijana huyo akitazama video za simu mahiri kwenye choo.