Mrembo ajilipa kwa kuchukua TV ya jamaa aliyekataa kumlipa baada ya kushiriki tendo

Baada ya kupunja raha usiku kucha, jamaa huyo alishindwa kumlipa mrembo huyo na kumbidi mrembo kuondoka na runinga, saa ya mkononi na vitu vingine vyote thamani ya 59,100.

Muhtasari

• Mwanamke huyo, ambayo amepewa jina la EWM, 38 pia alishtakiwa kwa kutoa Sh3,880 kutoka kwa akaunti ya Mpesa ya mwanaume huyo, JKM.

• Aliiba televisheni, saa na simu katika eneo la Masimba, Kayole Nairobi usiku wa Oktoba 24/25.

Mwanamke aliyefungwa jela pingu mikononi.
Mwanamke aliyefungwa jela pingu mikononi.
Image: Shutterstock

Mwanamke mmoja ambaye ni mchuuzi wa ngono jijini Nairobi amejipata pabaya baada ya kufikishwa mahakamani kwa shtaka la kuchukua vitu vya thamani vya mwanamume aliyekataa kumlipa baada ya kumgawia ‘tunda’.

Kwa mujibu wa toleo la Taifa Leo, mwanamke huyo alichukua runinga, saa ya mkononi na vitu vingine kutoka kwa mwanamume huyo ambavyo vinatajwa kuwa vya thamani ya elfu 59.

Mwanamke huyo, ambayo amepewa jina la EWM, 38 pia alishtakiwa kwa kutoa Sh3,880 kutoka kwa akaunti ya Mpesa ya mwanaume huyo, JKM.

Aliiba televisheni, saa na simu katika eneo la Masimba, Kayole Nairobi usiku wa Oktoba 24/25.

Korti ilielezwa kuwa JKM alikuwa akijiburudisha kwa kileo klabuni, mwanamke huyo alipofika akamwalika waketi meza moja ili wanywe pamoja.

Wawili hao kisha waliondoka na kuenda kwa nyumba ya EWM  lakini mwanamke akataka waongeze pombe ndipo tena wakaenda kwenye baa jingine na kununua pombe nyingi, Taifa Leo walielewa.

Waliporejea kwa nyumba na kuendelea kunywa, JKM aliomba azime kiu chake cha mapenzi lakini mwanamke huyo akasema lazima angelipwa Sh5,000 kwa huduma hiyo.

Anadai kuwa baada ya kugawiwa ‘vitu’ kishujaa, JKM alikataa kulipa na wawili hao wakalemewa na usingizi.

Mwanamke huyo aliwaeleza polisi kuwa JKM alimpa nambari yake ya siri ya Mpesa lakini akabaini alikuwa na pesa kidogo ambazo hazikufikisha Sh5,000 walizoelewana.

Baada ya kuamka saa moja asubuhi, mshukiwa alibeba televisheni na bidhaa nyingine kisha kuondoka. Aliwaambia polisi kuwa aliuza televisheni hiyo kwa mhudumu anayeuza vifaa vya kielektroniki.

Alikamatwa baada ya kuonekana kwenye baa moja ambapo walikuwa wakinywa na JKM.

Mbele ya Hakimu Mkuu  Tito Gesora, aliwaachiliwa kwa dhamana ya Sh40,000 au pesa taslimu Sh30,00 huku kesi hiyo ikitarajiwa itatajwa mnamo February 9 kabla ya kuanza kuskiziwa Juni 24 mwaka ujao.