Mwanamume mmoja katika jimbo la Florida nchini Marekani alikamatwa baada ya kudaiwa kujisaidia haja kubwa kwenye mzoga wa mnyama jamii ya panya aliyekufa katikati ya msongamano wa magari, kulingana na polisi.
Jamaa huyo alitambuliwa kwa jina Rudy Wilcox, 45, ana lichukuliwa na polisi wa Clearwater siku ya Jumatano karibu 5:30 p.m. baada ya kuonekana akiangusha suruali katikati ya makutano ya Barabara kisha akakata gogo kwenye mzoga mbele ya macho ya watu wanaoendesha magari."
"Jamaa alionekana akijisaidia haja kubwa kwenye mzoga wa mnyama aina ya possum huku suruali yake ikiwa imeshushwa na sehemu yake ya haja kubwa ikiwa wazi,” hati ya kiapo ya Kaunti ya Pinellas iliyopatikana na The Smoking Gun ilisomeka.
Alipoulizwa, Wilcox alikanusha mashtaka na kusema afisa aliyemshuhudia "Haoni sawa," kulingana na hati ya kiapo - lakini polisi hawakuwa nayo.
"Ushahidi wa kimaumbile ulitazamwa katika eneo la tukio ambao unathibitisha madai hayo," hati ya kiapo ilibainisha.
Wilcox, ambaye hana makazi, hakuwa chini ya ushawishi wa kilevi chochote wakati wa tukio linalodaiwa, kulingana na ripoti hiyo.
Alishtakiwa kwa kufichua viungo vya siri na kuzuiliwa katika rumande akisubiri uchunguzi Zaidi kufuatia tukio hilo la ajabu.