logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Safari ya ndege yatatizika angani mume akivua nguo kwa hasira wakigombana na mkewe

Abiria hao waliarifiwa mmoja mmoja kwamba ndege hiyo ingetua India.

image
na Radio Jambo

Makala01 December 2023 - 07:07

Muhtasari


• Mamlaka ya usalama wa anga ya Uwanja wa Ndege wa Delhi iliambia shirika la habari la India ANI:

• 'Sababu ya ugomvi kati ya mwanamume na mwanamke bado haijajulikana, lakini ndege ilibidi ielekezwe kutokana na ugomvi kati ya mwanamume na mwanamke.'

Ndege ya Ujerumani.

Wasafiri wa ndege ya shirika la ndege la Ujerumani, Lufthansa walipigwa na butwaa baada ya zogo la wanandoa safarini kuchukua mkondo usiotarajiwa.

Kwa mujibu wa Daily Mail, mwanamume alikuwa anagombana na mke wake ndani ya ndege kabla ya ugomvi wao kufikia kilele na mume huo kusimama na kuanza kuvua mavazi yake yote.

Mwanamume huyo kisha aliwasha blanketi moto huku akipiga kelele kwamba ‘nitaua mtu’ ndani ya ndege hiyo iliyokuwa inaelekea Bangok.

Marubani walilazimika kuchuka tahadhari na kutua ndege hiyo kwa ghafla mjini New Delhi, India kabla ya mwanamume huyo kutolewa nje kwa haraka.

Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 53, ambaye jina lake halijatajwa, alitolewa kwenye ndege ya Airbus A380 na wanajeshi mjini New Delhi baada ya ndege hiyo kulazimishwa kuacha njia iliyokuwa imepanga kutoka Munich hadi Bangkok mapema Jumatano asubuhi, Daily Mail waliripoti.

Mashahidi waliokuwa kwenye ndege ya Lufthansa LH772 walisema kisa hicho kilitokea ghafla baada ya mke wa mwanamume huyo raia wa Thailand kumwambia mfanyakazi kuwa alihisi 'kutishwa' na mumewe na kuwataka waingilie kati saa chache tu katika safari hiyo ya saa 10 na dakika 45.

Katika ghadhabu ya ajabu, abiria huyo alianza kurusha chakula, akajaribu kuchoma blanketi na njiti, akavunja simu yake na kuvua nguo, mashuhuda walisema. 'Nitawaua ninyi nyote!' aliripotiwa kusema, akipuuza maagizo kutoka kwa wafanyakazi wa cabin.

Walipokuwa wakikaribia India, marubani waliambia udhibiti wa trafiki wa anga kuhusu 'hali iliyo na abiria mkorofi' na mara moja wakapewa ruhusa ya kutua katika uwanja wa ndege wa Indira Gandhi International (IGI) katika mji mkuu wa India, ambako alikamatwa.

Abiria hao waliarifiwa mmoja mmoja kwamba ndege hiyo ingetua India.

Mamlaka ya usalama wa anga ya Uwanja wa Ndege wa Delhi iliambia shirika la habari la India ANI: 'Sababu ya ugomvi kati ya mwanamume na mwanamke bado haijajulikana, lakini ndege ilibidi ielekezwe kutokana na ugomvi kati ya mwanamume na mwanamke.'

Afisa wa Kurugenzi ya Usafiri wa Anga (DGCA) alisema kuwa Lufthansa sasa inaratibu na Ubalozi wa Ujerumani kuhusu abiria.

Lufthansa ilikiri katika taarifa kwamba ndege hiyo ilielekezwa Delhi kutokana na abiria mkorofi ndani ya ndege hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved