Pasta aliyewalaghai waumini wa kanisa lake Ksh 213M ajitetea kuwa ni Mungu alimtuma

Alisema kwamba wakati fulani Mungu alimjia ndoto na kumwomba afanye hivyo, naye akakubali kwamba yeye na mke wake walitumia pesa hizo katika “urekebishaji wa nyumba ambao Mungu alituambia tufanye.”

Muhtasari

• Bw. Regalado alisema kuwa hataki wawekezaji kuwa na "wazimu" kwa waendesha mashtaka.

Image: BBC

Mchungaji wa kanisa moja katika jimbo la Colorado nchini Marekani amewashangaza wengi baada ya kudai kwamba Mungu ndiye alimtuma kuwalaghai waumini wa kanisa lake Zaidi ya dola milioni 1.3 – sawa na milioni 213 za Kenya.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyowashangaza wengi kwenye jarida la The New York Times, pasta Eli Regalado na mke wake Kaitlyn walipandishwa mahakamani kwa dai la kuwauzia waumini wa kanisa lao hisa za biashara ya hela, INDXcoin kwa ahadi ya uwongo kwamba wawekezaji wanaonunua sarafu ya crypto watakuwa matajiri.

Hata hivyo kaitka kujitetea kwake, mchungaji huyo aliishangaza mahakama kwa vicheko baada ya kudai kwamba kila kitu ambacho alikifanya ni kufuata maagizo kutoka kwa Mungu.

Katika video iliyoonwa na jarida hilo akihutubia malalamiko hayo wiki jana, Bw. Regalado alisema kuwa hataki wawekezaji kuwa na "wazimu" kwa waendesha mashtaka.

"Lazima wafanye hivi," alisema. "Namaanisha, ikiwa unafikiria juu ya hili: Tuliuza sarafu ya siri bila njia ya kutoka wazi. Tulifanya. Tulimkubali Mungu kwa neno lake na tukauza sarafu ya siri bila njia ya kutoka wazi.”

Bw. Regalado alisema kuwa kwa sababu ya matatizo ya kubadilishana cryptocurrency, wawekezaji hawakuweza kuchukua fedha zao.

Bwana Regalado pia alisema kwenye video kwamba aliingia katika biashara ya cryptocurrency kwa sababu "Bwana" alimwambia.

Alisema kwamba wakati fulani Mungu alimjia ndoto na kumwomba afanye hivyo, naye akakubali kwamba yeye na mke wake walitumia pesa hizo katika “urekebishaji wa nyumba ambao Mungu alituambia tufanye.”

Ripoti hiyo pia ilimnukuu Bw. Regalado akisema bado ana matumaini kwamba wawekezaji wangeweza kurejeshewa pesa zao, na kwamba anaamini “Mungu atafanya muujiza katika sekta ya fedha.”