Mike Sonko atoa VAR ya kweli kuhusu picha inayoenezwa ya mwanamke nyuma yake

“Picha hiyo imehaririwa ili kuibua dhana kwamba ‘rosecoco’ ya mwanamke huyo inaonekana, ambapo si kweli,” aliongeza.

Muhtasari

• Kiongozi huyo wa zamani wa Nairobi alifichua kwamba kiti hicho kilikuwa kimehifadhiwa kwa ajili ya waziri Penina Malonza.

SONKO.
SONKO.
Image: X//SONKO MIKE

Wikendi iliyopita, watumizi wa mitandao ya kijamii nchini walizua minong’ono bada ya picha kuvujishwa kutoka kwa hafla ya jamii ya Anzauni kaunti ya Kitui ambayo gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko alihudhuria kama mmoja wa wageni waalikwa.

Katika picha hiyo iliyoenezwa pakubwa mitandaoni, Sonko alionekana ameketi akiwa nadhifu kama kawaida yake lakini nyuma yake, pembeni kushoto palionekana mwanamke ambaye alikuwa ameketi na kuonekana kuwa hakuwa amevalia mwanandani.

Mwanamke huyo nyuma ya Sonko aliifanya picha hiyo kuzua gumzo kubwa mitandaoni baadhi wakienda mbali Zaidi na kutoa ufafanuzi wa kina kana kwamba ni VAR inayochunguza madhambi ya wanasoka uwanjani.

Sonko aligutushwa na hilo na baadae katika mtandao wa X alichapisha mfululizo wa picha halisi ambazo alisema kuwa ni ‘VAR ya ukweli’ na kusema kwamba picha hiyo ilikuwa imehaririwa ili kumuonesha mwanamke wa watu kuwa alikuwa ‘bila’.

“Baada ya uchunguzi wa kina na kupitia picha asili zilizochukuliwa wakati wa hafla ya jamii ya Anzauni huko Kitui wikendi iliyopita ambapo nilikuwa mmoja wa wageni waalikwa, nimekuja kubaini kwamba picha inayodaiwa kuwa ya mwanamke nyuma yangu anayeonekana kuweka wazi nyeti zake si ya kweli, imehaririwa,” Sonko alisema kwa sehemu.

“Picha hiyo imehaririwa ili kuibua dhana kwamba ‘rosecoco’ ya mwanamke huyo inaonekana, ambapo si kweli,” aliongeza.

Kiongozi huyo wa zamani wa Nairobi alifichua kwamba kiti hicho kilikuwa kimehifadhiwa kwa ajili ya waziri Penina Malonza lakini wanawake mbalimbali walikikalia kwa muda tofauti tofauti akisubiriwa waziri huyo kufika.

Sonko alituhumu vikali yeyote ambaye alihusika katika kuhariri picha hiyo ili kuonesha kwamba mwanamke huyo alikuwa ‘bila’ na kusema kwamba ni mama ya watu ambaye ameathirika kwa njia hasi kutokana na picha hiyo kuenezwa.

“Hata kama mwanamke huyo simjui, sio tu kwamba yeye ni uso miongoni mwa umati bali pia ni mama ya watu, shangazi, binti au hata dada wa watu. Anastahili heshima. Kwa hivyo, ninatoa wito kwa yeyote ambaye anamfahamu kumjulisha kwamba ninamtafuta ilia je kwa ofisi yangu tuanzishe mkakati wa kuwatafutia huduma za ushauri nasaha pamoja na familia yake,” Sonko alitoa ombi.