Msichana mwenye jinsia mbili ahukumiwa miaka 24 kwenye gereza la wanaume

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 26 akikiri mashtaka yake alisema alimpiga chupa kichwani kijana mhandisi na kumuua papo hapo, akisema alichochewa na filamu ya Netflix.

Muhtasari

• Miezi minne mapema, Blake alitiririsha moja kwa moja akiua paka wa jirani na kuuweka mwili wake kwenye mashine ya kusagia.

• Alikuwa akizunguka-zunguka katika mitaa ya jiji hilo akiwa amevalia koti la kofia la mtindo wa kijeshi, na akiwa amebeba rucksack iliyokuwa na 'sanduku la mauaji'

Mwanamke aliyefungwa jela pingu mikononi.
Mwanamke aliyefungwa jela pingu mikononi.
Image: Shutterstock

Msichana muuaji aliyebadili jinsia atatumikia kwa angalau miaka 24 katika jela ya kiume kwa mauaji ya mhandisi wa BMW ambaye alimlenga bila mpangilio kama sehemu ya ndoto potofu ya ngono iliyochochewa na filamu isiyo ya kweli ya Netflix.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Scarlet Blake mwene umri wa miaka 26 alivunja chupa ya vodka juu ya kichwa cha Jorge Martin Carreno, akamnyonga kisha akamsukuma kwenye mto Cherwell huko Oxford, Uingereza.

Wakili wa utetezi wa Scarlet Blake alikiri mteja wake alikuwa hatari sana ambaye hakuna msamaha ungeweza kuhisi kuwa ni salama kumwachilia tena katika jamii.

Miezi minne mapema, Blake alitiririsha moja kwa moja akiua paka wa jirani na kuuweka mwili wake kwenye mashine ya kusagia.

Kakake Bw Carreno, Gerardo aliiambia Mahakama ya Oxford kwamba maisha ya ndugu yake yameibiwa na muuaji huyo, na kuongeza: 'Hatujalala usiku na mchana. Kupitia uchungu wa kufiwa na mwana na kaka ni changamoto ambayo familia haiwezi kukabili.' – Daily Mail walieleza.

Mama yake, Carmen, alisema kufiwa na mwanawe mpendwa kutaacha 'jeraha wazi' katika familia.

Blake, ambaye wazazi wake ni madaktari wanaoheshimika, alimlenga mfanyakazi wa BMW mwenye umri wa miaka 30 alipokuwa akitoka katika klabu cha usiku huko Oxford mnamo Julai 24, 2021 - Jumamosi ya kwanza usiku baada ya vizuizi vya Covid kupunguzwa, taarifa hiyo ilisema.

Alikuwa akizunguka-zunguka katika mitaa ya jiji hilo akiwa amevalia koti la kofia la mtindo wa kijeshi, na akiwa amebeba rucksack iliyokuwa na 'sanduku la mauaji' lililokuwa na kamba ya gauni ya garrotte na chui.