David Ndii ajigamba kuhusu mkewe baada ya kuhusishwa kimapenzi na mwanadada mwingine

Ndii alichukua hatua hiyo baada ya wanamitandao kumshtumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine.

Muhtasari

•David Ndii amemuonyesha kwa fahari mke wake kwenye mtandao wa kijamii wa X baada ya kushutumiwa kwa kukosa uaminifu.

•"Nachumbiana na mpenzi huyu, pekee," David Ndii alisema chini ya picha zake na mke wake Mwende Gatabaki.

amemuonyesha kwa fahari mke wake Mwende Gatabaki
David Ndii amemuonyesha kwa fahari mke wake Mwende Gatabaki
Image: TWITTER// DAVID NDII

Mwenyekiti wa Baraza la Rais la Washauri wa Kiuchumi David Ndii amemuonyesha kwa fahari mke wake kwenye mtandao wa kijamii wa X baada ya kushutumiwa kwa kukosa uaminifu.

Huku akijibu shutuma za kuwa na mpenzi mwingine siku ya Jumapili, mwanauchumi huyo alichapisha picha yake na mkewe Mwende Gatabaki na kusisitiza kuwa mwanamke huyo aliyekuwa mgombea wa ugavana kaunti ya Kiambu ndiye mwanamke pekee moyoni mwake.

"Nachumbiana na mpenzi huyu, pekee," David Ndii alisema chini ya picha zake na mke wake Mwende Gatabaki.

Ndii alichukua hatua hiyo baada ya wanamitandao kumtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine.

"Kwa hivyo  M***age unatoka kimapenzi na Ndii, mtandao huu una njia ya kuvujisha siri zako bila kujua, unahitaji tu kusoma kati ya mistari," mtumiaji wa Twitter alidai.

Katika jibu lake, Ndii alipuuzilia mbali madai hayo akisema, "M***age ni nani?"

Mshauri huyo wa masuala ya kiuchumi wa Rais William Ruto zaidi alichapisha picha zingine kadhaa za kumbukumbu zake na mkewe kuthibitisha safari yao pamoja na kujitolea kwake kwa mapenzi yao.

Ndii ni miongoni mwa watu maarufu ambao wamekabiliwa na shutuma na mashambulizi mengi kwenye mitandao ya kijamii siku za hivi majuzi.

Mwezi uliopita tu, alikuwa akizungumziwa mtandaoni baada ya picha yake akitembea kando ya Rais William Ruto kusambazwa sana mtandaoni.

Katika picha, mwanauchumi huyo mkuu alikuwa akitembea kwa miguu pamoja na Rais Ruto huko Naivasha ambapo walikuwa wakihudhuria Retreat ya Kitaifa.

Maoni mengi yalikuwa yale ya kulinganisha uzito wake wa sasa na hapo awali.

Ndii ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Rais la Washauri wa Kiuchumi, aliwajibu Wakenya akiwakashifu wakosoaji wa mwili wake.

"Kuwa na uzito kupita kiasi ni changamoto ya kibinafsi inayoweza kurekebishwa isiyo na madhara kidogo au isiyo na matokeo yoyote kwa umma kwa ujumla. Kuwa mtupu ni mzigo usiotibika kwa jamii. Ũrimũ ndũrĩ ndawa. Kuwa na wapumbavu wengi bila kitu bora kuzungumza kwenye jukwaa la umma ni shida kubwa. janga la kitaifa,"

Watumizi wengine wa Twitter pia walitoa maoni kuhusu uzito wa mwili wake na kuwafurahisha Wakenya huku wakikisia kwa nini Ndii alikuwa mkubwa zaidi.