Mwanamume afunga ndoa na mmoja wa mapacha wenye mwili mmoja lakini vichwa tofauti

Mapacha hao hushiriki mwili mmoja, na kutoka kiuno kwenda chini, viungo vyao vyote, ikiwa ni pamoja na utumbo, kibofu na viungo vya uzazi, wana’share.

Muhtasari

• Katika filamu iliyorekodiwa wasichana hao walipokuwa matineja, mama yao alisema walikuwa na hamu ya kupata watoto wao wenyewe siku moja.

Pacha mmoja wa walioshikana aolewa.
Pacha mmoja wa walioshikana aolewa.
Image: Hisani

Mwalimu wa Marekani ambaye alijipatia umaarufu katika kipindi cha televisheni cha uhalisia akiwa na pacha wake ameripotiwa kufunga ndoa kimya kimya miaka mitatu iliyopita

Kulingana na rekodi za umma zilizopatikana na US TODAY, Abby Hensel, ambaye sasa ana umri wa miaka 34, kutoka Minnesota, alifunga pingu za maisha na Josh Bowling, muuguzi na mkongwe wa jeshi mnamo 2021.

Abby na dadake Brittany, mmojawapo wa seti chache tu za mapacha wa dicephalus katika historia walisalimika wakiwa wachanga, walipata umaarufu kwenye onyesho lao la TLC ambalo liliandika matukio yao makuu ya maisha, ikiwa ni pamoja na kuhitimu kwao shule ya upili na kutafuta kazi.

Mapacha hao hushiriki mwili mmoja, na kutoka kiuno kwenda chini, viungo vyao vyote, ikiwa ni pamoja na utumbo, kibofu na viungo vya uzazi, wana’share.

Katika filamu iliyorekodiwa wasichana hao walipokuwa matineja, mama yao alisema walikuwa na hamu ya kupata watoto wao wenyewe siku moja, akieleza: 'Pengine hilo ni jambo ambalo linaweza kufanya kazi kwa sababu viungo hivyo vinafanya kazi kwa ajili yao.'

"Ndio, tutakuwa mama," Brittany alikubali.

Katika mahojiano mengine, Brittany alisisitiza hamu yao ya kuwa na familia zao wenyewe, akisema: 'Ulimwengu mzima hauhitaji kujua tunaona nani, tunafanya nini na tutafanya wakati gani. Lakini niamini, sisi ni watu tofauti kabisa.'

Abby aliongeza: 'Ndio, tutakuwa akina mama siku moja, lakini hatutaki kuzungumza kuhusu jinsi itafanya kazi bado.

Kwenye akaunti ya TikTok @abbyandbrittanyhensel, video ilichapishwa hivi majuzi ikionyesha siku ya harusi ya Abby - na akaunti ya Facebook yenye jina Britt And Abby pia ilikuwa na picha ya wanandoa hao wenye furaha.