Mwanamume ajiweka sokoni na kutangaza kujiuza kutokana na hali ngumu ya kiuchumi (Video)

Alifichua kwamba sasa anaishi katika jengo ambalo halijakamilika.Pia alidai kuwa watoto wake wako na mama yao kijijini kwa vile hana uwezo wa kuwatunza mjini.

Muhtasari

• Video hiyo imeibua hisia mseto, baadhi wakimtaka kuhamia kijijini kama mjini maisha yamekuwa mbinde kwake huku wengine wakishindwa jinsi atanunuliwa ima kama mtumwa au kijakazi

Mwanamume atangaza kujiuza
Mwanamume atangaza kujiuza
Image: Screengrab

Mwanamume wa umri wa makamo raia wa Ghana anayeitwa Samuel Mensah amekuwa gumzo kwenye anga ya kidijitali baada ya kujiweka sokoni akitangaza kujiuza ka kile alikitaja kuwa ugumu wa maisha.

Akizungumza katika mahojiano na mwanablogu moja kwa lugha ya kiasili nchini humo, Mensah alifichua kwa masikitiko kwamba maisha yamemwendea kinyama hivyo ameona ni busara kujiweka sokoni.

Katika mahojiano ya kusikitisha ambayo tangu wakati huo yameibua hisia, Mensah alifichua kwamba sasa anaishi katika jengo ambalo halijakamilika.

Pia alidai kuwa watoto wake wako na mama yao kijijini kwa vile hana uwezo wa kuwatunza mjini.

Katika dakika za mahojiano, Mensah alitoa nambari yake kwa wanunuzi wake wawasiliane naye.

Video hiyo imeibua hisia mseto, baadhi wakimtaka kuhamia kijijini kama mjini maisha yamekuwa mbinde kwake huku wengine wakishindwa jinsi atanunuliwa ima kama mtumwa au kijakazi.

“Nani amemlipa kufanya hivi....? Anaweza kwenda kufua au kupiga pasi nguo, alichonacho ni mkweli....Kama Accra ni ghali ahame....Mpe kazi leo na ataacha baada ya miezi 2 akisema malipo hayatoshi. .....” mmoja alisema.

“"Kununua" inapaswa kunukuliwa vizuri aeleze anataka kununuliwa kivipi, kwa njia gani,” mwingine alihoji.

Tazama video hapa chini kujua zaidi...