Wanawake wavamia ekari 10 za shamba la Miraa na kung'oa wakidai imeharibu wanaume wao

" Sisi ni wajane kwa sababu ya hii muguka, wamekula wengine wakapatwa na saratani wakakufa juu ya sigara na hizi pombe, tumekataa sisi kama wanawake.”

Muhtasari

• " Sisi ni wajane kwa sababu ya hii muguka, wamekula wengine wakapatwa na saratani wakakufa juu ya sigara na hizi pombe, tumekataa sisi kama wanawake.”

Tanzania yateketeza shamba la miraa.
Tanzania yateketeza shamba la miraa.
Image: STAR

Makumi ya wanawake kutoka kijiji cha Oronie, kaunti ndogo ya Kajiado ya Kati kaunti ya Kajiado wamevamia shamba lenye ekari 10 za zao la miraa na kuiharibu kwa kuing’oa kwa ghadhabu katika kile wanadai mumea huo umewaharibia wanaume wao.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyopeperushwa kwenye runinga ya KBC1, wanawake hao walidai zao hilo limekuwa chanzo cha matatizo katika eneo lao, haswa kwa kuwaharibu wanaume ambao wamekuwa zuzu.

Wanawake hao pia walielekea katika kituo cha Enkorika kwenye kaunti hiyo ndogo na kufunga baadhi ya vilabu vya kuuza pombe kabla ya kuonekana wakiharibu pombe zenyewe kwa kupasua chupa na kuchoma.

“Sana sana chifu wa Orinie, atusaidie sababu tunaumia tukiwa wanawake. Sisi ni wajane kwa sababu ya hii muguka, wamekula wengine wakapatwa na saratani wakakufa juu ya sigara na hizi pombe, tumekataa sisi kama wanawake.”

“Tunaomba usaidizi wenu nyinyi kama serikali leo muingililie hili jambo lipate kutokomezwa hapa,” wanawake hao waliteta.