Mwanamke anayefuga ‘nyoka wa pesa’ avunja kimya, aeleza jinsi alimpata (video)

“Mimi jina ambao nimempa maaluma ni ‘nyoka wa pesa’. Huyu sio nyoka wa kawaida, ni nyoka wa kimiujiza. Nyoka huyu ni wa kunisaidia kitu kimoja tu; kuniletea pesa wakati nazihitaji, yeye hali chakula,” alifafanua Zaidi.

Muhtasari

• Mrembo huyo kwa jina Tiffah alieleza jinsi aliunganishwa na mtoa nyoka hao wa pesa na kisha akamkabidhiwa na kupewa masharti ambayo hata hivyo alisita kuyafichua.

• Hata hivyo, mrembo huyo alisema kuwa kuna kiwango ambacho wamewekewa cha pesa ambacho akitamka maneno yake ya siri kwa nyoka anazipata.

Mrembo anayefuga nyoka wa pesa
Mrembo anayefuga nyoka wa pesa
Image: screengrab//Bongo Touch

Mwanamke mmoja mwenye umri wa makamo amewashangaza watu baada ya kukiri kwamba anamfuga nyoka wa ajabu ambaye anamtamkia maneno Fulani kabla ya kupata pesa.

Mrembo huyo kutoka Tanzania alifanya mahojiano na blogu ya Bongo Touch na kumuonyesha kabisa nyoka huyo mkubwa ambaye alisema kuwa si nyoka wa kawaida.

Mrembo huyo kwa jina Tiffah alieleza jinsi aliunganishwa na mtoa nyoka hao wa pesa na kisha akamkabidhiwa na kupewa masharti ambayo hata hivyo alisita kuyafichua.

“Tulienda na ndio huko nilikopata mafanikio yangu na rafiki yangu pia ndiko alipata ya kwake mafanikio. Huyu ni nyoka ambaye masharti nilipewa na mtaalamu, kuna maneno ambayo natakiwa niseme, yale maneno nikiyasema huwa nampata, namuona halafu nikisema hayo maneno pia ninapata pesa kwa ule wakati ambao nazihitaji,” alisema.

Hata hivyo, mrembo huyo alisema kuwa kuna kiwango ambacho wamewekewa cha pesa ambacho akitamka maneno yake ya siri kwa nyoka anazipata.

“Siwezi kukutajia kiwango cha pesa ambacho nakihitaji kutoka kwa yule nyoka, hiyo ni siri yangu, na kiwango hicho siwezi kukivuka. Maneno ambayo ninaongea kwa nyoka huyu si lugha yetu ambayo tunaitumia, ni lugha maaluma nilipewa na mtaalamu.”

“Mimi jina ambao nimempa maaluma ni ‘nyoka wa pesa’. Huyu sio nyoka wa kawaida, ni nyoka wa kimiujiza, ili aje kwangu kuna maneno ambayo natamka nimpate na kuna yenye natamka aondoke. Nyoka huyu ni wa kunisaidia kitu kimoja tu, kuniletea pesa wakati nazihitaji, yeye hali chakula,” Tiffah alifafanua Zaidi.

Kuhusu masharti, mrembo huyo alisema kwamba kuna muda anahitajika kutoa pesa ili kununua kitu Fulani na kuna muda mwingine hatakiwi kutoa kabisa hata senti ili kupata kitu Fulani.

Tazama video hiyo hapa chini kisha utoe maoni yako;

Mrembo anayefuga nyoka wa pesa
Mrembo anayefuga nyoka wa pesa
Image: screengrab//Bongo Touch