Ni mimi nilianza kuvaa Kaunda, sasa Ruto amepatia nguo hii jina mbaya – Seneta Onyonka

Seneta huyo alisema kwamba ni wakati taifa ligutuke kutoka usingizini na viongozi kufahamu kwamba Gen Z wako macho na wanafuatilia kila kitu, tofauti na vizazi vya awali ambavyo havikuwa vinafuatilia mienendo ya viongozi wao.

Muhtasari

• “Gen Z wako macho, siku hizi wanakufuatilia, wanaweza kujua ni ndege ipi ya kibinafsi ulichukua, ilienda wapi na lini ilirudi. Ni wakati tufahamu kwamba kuna sherrif mpya mjini,” aliongeza.

Seneta Onyonka adai kuwa wa kwanza kuibuka na kaunda suti
Seneta Onyonka adai kuwa wa kwanza kuibuka na kaunda suti

Seneta wa Kisii Richard Onyonka amedai kwamba rais William Ruto amechafua jina zuri la vazi la Kaunda, ambalo anadai yeye ndiye mwanasiasa wa kwanza wa kizazi kipya Kenya kuanza kuvaa vazi hilo katika shughuli rasmi.

Akizungumza kwenye bunge la seneti Jumatano wakati wa kikao cha kujadili hali ambayo taifa limejipata ndani mwake kufuatia maandamano ya vijana wa Gen Z wanaopinga serikali, alisema kwamba jambo pekee linalomfanya kumkasirikia rais Ruto ni jinsi ambavyo amefanya Kaunda suti kuonekana mbaya kwa Wakenya.

Rais Ruto tangu alipochukua hatamu za uongozi kama rais miaka miwili iliyopita, alikumbatia mavazi ya Kaunda na tangu wakati huo limekuwa kama moja ya nembo ya uongozi wake.

Hata hivyo, Onyonka anadai ndiye aliyeanza kuvaa vazi hilo lakini sasa anasikitika jinsi limeanza kuhusishwa kwa dhana mbaya kisa limekuwa likitumiwa na rais Ruto.

Onyonka alikuwa akizungumza jinsi taifa linastahili kuendeshwa kwenda mbele, aliwasihi maseneta wenzake kwamba ni wakati wakubali wanaweza vaa Kaunda suti na hata kuendesha magari madogo ya bei rahisi.

“Sisi katika jumba hili ni wakati tuanze kuamini kwamba tunaweza kupunguza mishahara yetu, tumiliki magari madogo na hata tuvae Kaunda suti. Kusema kweli kitu pekee ambacho kinaniudhi kuhusu rais Ruto ni kwamba, mimi ndiye niliyeanza kuvaa Kaunda suti, sasa amepatia Kaunda jina baya. Nataka Wakenya kupenda Kaunda jinsi ninazipenda,” seneta Onyonka alisema.

Seneta huyo alisema kwamba ni wakati taifa ligutuke kutoka usingizini na viongozi kufahamu kwamba Gen Z wako macho na wanafuatilia kila kitu, tofauti na vizazi vya awali ambavyo havikuwa vinafuatilia mienendo ya viongozi wao.

“Gen Z wako macho, siku hizi wanakufuatilia, wanaweza kujua ni ndege ipi ya kibinafsi ulichukua, ilienda wapi na lini ilirudi. Ni wakati tufahamu kwamba kuna sherrif mpya mjini,” aliongeza.