Mwili wa mwanamume umepatikana miaka 22 baada ya kutoweka akikwea mlima

William aliripotiwa kutoweka mnamo Juni 2002, akiwa na umri wa miaka 59, wakati maporomoko ya theluji yalipozika ziara yake kwenye Mlima huo wa urefu wa zaidi ya futi 22,000.

Muhtasari

• Stampfl alikufa na marafiki zake Matthew Richardson na Steve Erskine mnamo Juni 2002

• Mwili wa Stampfl, pamoja na nguo zake, kamba na buti ulikuwa umehifadhiwa vyema na baridi, kulingana na picha zilizosambazwa na polisi.

• Pasipoti yake ilipatikana miongoni mwa mali zake, na kuruhusu polisi kutambua mwili huo.

Mlima Everest
Mlima Everest
Image: Hisani

Mwili wa mpanda milima wa Marekani ambaye alitoweka miaka 22 iliyopita alipokuwa akijaribu kukwea vilele vya juu zaidi katika mlima Andes umepatikana.

William Stampfl aliripotiwa kutoweka mnamo Juni 2002, akiwa na umri wa miaka 59, wakati maporomoko ya theluji yalipozika ziara yake kwenye Mlima Huascaran, ambao una urefu wa zaidi ya futi 22,000. Juhudi za utafutaji na uokoaji hazikuzaa matunda.

Polisi katika eneo la Ancash nchini Peru walipata mwili wake siku ya Ijumaa katika safu ya Cordillera Blanca, karibu na kambi ya futi 17,060 juu ya usawa wa bahari, baada ya kufichuliwa na kuyeyuka kwa barafu iliyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mwili wa Stampfl, pamoja na nguo zake, kamba na buti ulikuwa umehifadhiwa vyema na baridi, kulingana na picha zilizosambazwa na polisi.

Pasipoti yake ilipatikana miongoni mwa mali zake, na kuruhusu polisi kutambua mwili huo.

Mabaki yake yaliletwa mlimani mwishoni mwa juma na waongozaji na maafisa wa polisi na kuwekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika mji wa Huaraz.

Milima ya kaskazini-mashariki mwa Peru, nyumbani kwa vilele vya theluji kama vile Huascaran na Cashan, inapendwa na wapanda milima kutoka kote ulimwenguni.

Mamia ya wapandaji hutembelea mlima huo kila mwaka wakiwa na waelekezi wa mahali hapo, na huwachukua takriban wiki moja kufika kileleni.

Stampfl alikufa na marafiki zake Matthew Richardson na Steve Erskine walipojaribu kupanda mwaka wa 2002.

Mwili wa Erskine ulipatikana muda mfupi baada ya maporomoko hayo, lakini wa Richardson bado haujapatikana.

 

Kumekuwa na ongezeko la ugunduzi wa mabaki ya wapandaji milima waliokosekana, watelezi na wapandaji huku barafu zikizidi kuyeyuka duniani kote.