•Salasya ametangaza kwamba anatafuta msichana wa kumpikia .
•Amesema lazima mwanadada huyo awe Gen-z.
Kwa mara tena Mbunge mcheshi wa Mumias mashariki Peter salasya,kupitia ukurasa wake wa facebook amedokeza kupitia video kuwa, yupo tayari kwa mara ya kwanza kuajiri msichana wa kazi.
Hii ni kutokana na kile ambacho amesema kuwa wapishi wake ambao ni wanaume wamekuwa wakimpikia ugali sukuma kila siku.
"Nimechoka kupikiwa ugali na sukuma kila siku na wanaume wezangu " alisema kwenye video.
Aidha Salasya kwenye video hiyo, amezitaja sifa za kijakazi anayetafuta huku akisema kuwa lazima awe Gen-z na muraibu wa mapishi.
Ikumbukwe, hapo awali Salasya aliwahi kuweka bayana kwamba anatafuta mke.
"Hii baridi inaanza kunilazimisha kuanza kufikiria kupata mwanamke mmoja mwaka huu alafu mwingine mwaka ujao," alafu.
Salasya kutokuwa na mke ni jambo ambalo huibua mijadala anapokua kwenye umma, huku baadhi ya wanadada wakichukua fursa ya kubeba vibango vyenye maandishi "naomba unioe salasya ".
Aidha salasya amekuwa na msimamo dhabiti wa kuwa yeye yupo tayari kufunga ndoa na mwanadada ambaye ni mwalimu na ambaye pia ni bikira.
Hili lilijitokeza wakati PK alipatana na Bi Lavyn Shantell ambaye alitaka sana wawe kwenye mahusiano na kusema kua yuko shwari kufunga ndoa na Salasya .