logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Terence Creative kusimamia 'honeymoon' ya Sherman na Kendi

Wanandoa hao walipata umakini baada ya kufichua hadithi yao ya upendo.

image
na Davis Ojiambo

Habari23 August 2024 - 13:33

Muhtasari


  • •Mbunifu wa maudhui Terence Creative amesema atasaidia safari ya mwanzo ya harusi (honeymoon) ya Tony Sherman na Kendi.
  • •Tony na Kendi walipatana wakati wa maandamano ya kupinga serikali na wakapendana.
  • •Wawili hao wamepanga kufanya harusi tarehe 25, Agosti katika jiji la Nairobi.
Sherman Tony, Kendi the maandamano couple

Mbunifu wa maudhui Terence Creative amesema ameahidi kusaidia safari ya mwanzo ya harusi (honeymoon) ya Tony Sherman na Kendi. Wawili hao walikutana wakati wa maandamano ya kupinga serikali na wameamua kuoana Junapili, Agosti 25.

Terence atasaidia kushirikiana na Bonfire Adventures ili kutuma wanandoa hao Mombasa baada ya harusi.

Wanandoa hao walipata umakini baada ya kufichua hadithi yao ya upendo ya kipekee.Walikutana wakati wa maandamano ya kupinga serikali jijini Nairobi na mara moja wakapendana.

Baada ya miezi mitatu, Sherman alipendekeza na sasa wamepanga kuoana. Shermanna Kendi wamekusudia kuoana Jumapili Agosti 25, katika sherehe ya umma kwenye eneo hilo ambapo walikutana mara ya kwanza.

Kwa video iliyoshirikishwa na Sherman Tiktok, Terence Creative alieleza msaada wake kwa wanandoa hao na kutangaza ya kwamba ataongea na Bonfire Adventures ili kusaidia safari ya mwanzo ya harusi.

Kwenye video Terence amesikika akisema "Honeymoon tutakuweka pale Mombasa.....Congratulation Sherman Tony, na salimia mama sana...kwa hivyo honemoon ni kwangu......Nitasimamia hiyo.......honeymoon ni mimi nasimamia....nitawasimamia na Bonfire."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved