Mwanasoka wa zamani avunja kimya baada ya kufutwa kazi BBC

Alikiri alituma "jumbe zisizostahili" kwa wafanyakazi wenzake wawili katika kipindi cha the One Show.

Muhtasari

•Alisisitiza "hakufanya chochote kilicho kinyume cha sheria" na kwamba alituma jumbe hizo kwa "watu wawili wazima walioridhia".

•Mkataba wa Jenas ulisimamishwa wiki hii kwa madai ya kutuma ujumbe usiofaa kwa mfanyakazi mwenzake mwanamke.

Image: BBC

Mchezaji wa kandanda wa zamani na mtangazaji Jermaine Jenas ameliambia gazeti la the Sun kwamba "anajutia" na kwamba "amewaangusha na kuwafeli watu wengi" baada ya kufutwa kazi kama mtangazaji wa BBC.

Aliambia gazeti hilo kwamba alituma "jumbe zisizostahili" kwa wafanyakazi wenzake wawili katika kipindi cha the One Show, lakini akasisitiza kwamba "hakufanya chochote kilicho kinyume cha sheria" na kwamba alituma jumbe hizo kwa "watu wawili wazima walioridhia".

Mkataba wa Jenas ambaye alikuwa akitangaza vipindi vya ‘Match of the Day’ na ‘One Show’ ulisimamishwa wiki hii kwa madai ya kutuma ujumbe usiofaa kwa mfanyakazi mwenzake mwanamke.

BBC haijatoa taarifa zaidi kuhusu madai dhidi yake.

Jenas alianza rasmi taaluma ya kucheza kandanda akiwa na umri wa miaka 17, ambapo alichezea timu ya Nottingham Forest, ikifuatiwa na Newcastle United na Tottenham Hotspur.

Alichezea timu ya England mara 21 na kustaafu mwaka 2016, kabla ya kuingia katika utangazaji.