Spika Moses Wetang’ula ‘Papa wa Roma’ afurahi kukutana na Papa Francis, nchini Italia

Wetang’ula kwa muda mrefu amekuwa akitaniwa kwa jina ‘Papa wa Roma’, jina ambalo hata yeye mwenyewe ameonekana kulikubali na hata kulitumia kwenye chapisho hilo chini ya alama ya reli.

Spika Wetang'ula akutana na Papa Francis
Spika Wetang'ula akutana na Papa Francis
Image: x

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula amedhihirisha furaha yake baada ya kukutana na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis nchini Italia.

Wetang’ula, ambaye wengi wanamtania kwa jina la ‘Papa wa Roma’ alichapisha picha akisalimiana na Papa Francis wakati wa ziara yake katika kasri la Vatican.

“Akiwa na heshima ya kukutana na Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, katika Ikulu yake ya Kitume maarufu kwa jina la Kasri la Papa katika mji wa Vatican,” Wetang’ula alisema.

Alimsifia kiongozi huyo wa kanisa Katoliki akisema kuwa ni taswira kamili ya uongozi wa busara na wa kuwatumikia watu wa maisha ya chini, akitolea mfano juhudi zake za kushusha fursa za huduma za kibinadamu kwa watu wa chini.

“@Pontifex ni mfano wa Kiongozi wa kweli wa Mtumishi, akienda kwa nia yake ya kuleta matumaini, usawa na fursa kwa wasiobahatika. Pia anaonyesha ishara ya mfano wa kuigwa wa huruma, upendo, huruma na ujasiri anapoongoza kanisa la ulimwengu wote,” Wetang’ula alieleza.

Wetang’ula kwa muda mrefu amekuwa akitaniwa kwa jina ‘Papa wa Roma’, jina ambalo hata yeye mwenyewe ameonekana kulikubali na hata kulitumia kwenye chapisho hilo chini ya alama ya reli.