Shame on you kwa Gen Z wote mnaoomba Raila kushindwa katika kinyang’anyiro cha AUC

Gen Z katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakipiga kampemi wakitaka Odinga kushindwa, kwa kile wanahisi kwamba alisaliti maandamano yao yaliyolenga kumsinikiza rais Ruto kung’atuka mamlakani

Muhtasari

• Hivi majuzi, rais William Ruto alizindua rasmi kampeni za Odinga katika hafla iliyofanyika kwenye ikulu na kushuhudiwa na marais mbalimbali kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.

RAILA ODINGA.
RAILA ODINGA.
Image: FACEBOOK

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa amewasuta vijana wa Gen Z ambao wamekuwa wakiendeleza kampeni katika mitandao ya kijamii wakitaka Raila Odinga kuangushwa katika kinyang’anyiro cha mywenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika, AUC.

Odinga atakuwa anamenyana na wenzake wanne katika kinyang’anyiro hicho kitakachofanyika mwezi Februari mwaka 2025.

 “Kwa Gen Z na Wakenya wote wanaomtakia Tinga @RailaOdinga bahati mbaya aibu juu yako! Kuweni wazalendo majamaa!. Kelele nyingi kwenye mitandao ya kijamii na hakuna kitu mnasema hata,” Barasa aliasuta.

Hivi majuzi, rais William Ruto alizindua rasmi kampeni za Odinga katika hafla iliyofanyika kwenye ikulu na kushuhudiwa na marais mbalimbali kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.

Hata hivyo, baadhi ya vijana wa Gen Z katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakipiga kampemi wakitaka Odinga kushindwa, kwa kile wanahisi kwamba alisaliti maandamano yao yaliyolenga kumsinikiza rais Ruto kung’atuka mamlakani, na badala yake akaonyesha ushirikiano naye.

Ni kampeni ambazo Didmus Barasa amezitaja kuwa kama dua la kuku ambalo halimpati mwewe, akisema ni kelele za mitandaoni tu kwani hazitoathiri kwa njia yoyote matokeo ya Odinga katika kuwania wadhifa wa AUC.