Wachuuzi wa ngono na wanaume mashoga waeleza kwa nini hawapendi kutumia kondomu

Nchini Kenya, kuna takribani wanawake 197,000 wanaofanya biashara ya kuuza ngono huku wanaume 51,000 wakiwa wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao.

Muhtasari

• Nchini Kenya, kuna takribani wanawake 197,000 wanaofanya biashara ya kuuza ngono huku wanaume 51,000 wakiwa wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao.

• Ripoti hiyo inaonyesha kwamba wanawake 15,271 wanaofanya biashara ya kuchuuza ngono wanaishi jijini Nairobi.

Kenya yakabiliwa na uhaba wa kondomu
Kenya yakabiliwa na uhaba wa kondomu
Image: BBC

Wanawake wanaochuuza ngono pamoja na wanaume wa jumuiya ya LGBTQ wamefunguka sababu zao za kutopenda kutumia mipira ya kuzuia maambukizi.

Katika ripoti hiyo iliyochapishwa kwenye gazeti la The Star, utafiti vhuo ulifanyika katika jiji la Nairobi maeneo ambapo biashara hiyo huendeshwa.

Utafiti ulifanyika kati ya Aprili na Mei mwaka jana katika vituo 28 jijini Nairobi ambapo biashara ya ngono hufanyika.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kitaifa kuhusu maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini Kenya, kuna takribani wanawake 197,000 wanaofanya biashara ya kuuza ngono huku wanaume 51,000 wakiwa wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba wanawake 15,271 wanaofanya biashara ya kuchuuza ngono wanaishi jijini Nairobi.

Kwa mujibu wa The Star, idadi kubwa ya wachuuzi hawa wa ngono hawapendi kutumia kinga wakati wa kushiriki mapenzi, kizingiti kikubwa kikiwa ni ukosefu wa elimu ya kijamii.

Ripoti hiyo inasema pia kwamba wengi hupata ugumu kusafiri maeneo ya mbali kufikia kliniki za kuuza mipira ya kondomu, uhaba wa mipira ya kondomu ya bila malipo na pia unyanyapaa wanaopata wanapotembelea vituo vya afya ni baadhi ya sababu zingine zinazopunguza matumizi yao ya kondomu.

“Nafikiri wanaotoa elimu wako sawa, napenda huduma zao. Wanahitaji tu kupata mafunzo zaidi kwa sababu unajua naweza kuwa nina msongo wa mawazo, au naweza kuwa na mtatizo ya kisaikolojia,” alisema mwanamume mmoja anayefanya mapenzi na wanaume wenzake.

“Nafikiri ni vizuri walete hizi huduma karibu na sisi kwa sababu kutembelea vituo hivyo mbali pia ni gharama kubwa. Wakati mwingine hata unaweza kosa nauli. Hivyo ni afueni kama hizi huduma zitaletwa karibu na sisi ili kuturahisishia ufikiaji wa matibabu,” aliongeza mrembo anayechuuza ngono.