logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Anataka handshake,'Omanga na Cherargei wakosoa hatua ya Raila kufanya mkutano Kamukunji

Omanga, hata hivyo, alisema Rais Ruto si kama Rais wa zamani Uhuru Kenyatta

image
na Radio Jambo

Burudani23 January 2023 - 10:09

Muhtasari


  • Omanga alisema Raila anajaribu kushinikiza hendisheki kupitia maandamano yake na kwamba hatakoma hadi Rais William Ruto atakapompa kipaumbele.
Seneta mteule Millicent Omanga

Aliyekuwa seneta mteule Millicent Omanga amekashifu hatua ya kiongozi wa Azimio, Raila Odinga kufanya mkutano katika uwanja wa Kamukunji.

Omanga alisema Raila anajaribu kushinikiza hendisheki kupitia maandamano yake na kwamba hatakoma hadi Rais William Ruto atakapompa kipaumbele.

"Wazo la kuendelea kwa vitisho vya maandamano ni kujaribu kuishinikiza serikali katika hali ya hendisheki. Hataacha hadi Rais ampe tahadhari hiyo," alisema.

Omanga, hata hivyo, alisema Rais Ruto si kama Rais wa zamani Uhuru Kenyatta ambaye alifanya hendisheki  na Raila.

"Huyu wa sasa sio kama ule wa kitambo. Hii ilishaenda!"

Seneta wa Nandi Seneta Samson Cherargei akizungumziaa mkutano huo sasa anadai kuwa mikutano iliyopangwa ya kinara wa Azimio Raila Odinga ni njama ya kutaka hendisheki na Rais William Ruto.

Katika taarifa ya Jumatatu, seneta huyo alisema madai ya handshake ya  lazima haitafanyika.

Tinga alingoja hadi vitu vya devt vipelekwe nyanza sasa anaanza kuwachochea watu wake wachache dhidi ya serikali. Huu ni usaliti wa hendisheki kwa kulazimishwa jambo ambalo halitatokea Polisi LAZIMA washughulikie kwa ukatili waporaji wa mali za wananchi wakati wa mkutano wa kamukunji leo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved