Mwanamke awashangaza wengi kwa kujioa mwenyewe miaka 49 baada ya kutengana na mumewe

"Nilisema, unajua nini, nimefanya kila kitu kingine. Kwa nini isiwe hivyo? Nitajioa mwenyewe," alisema Dorothy.

Muhtasari

•Dorothy Fedeli alijioa mwenyewe siku ya Jumamosi katika harusi ndogo iliyoshuhudiwa na majirani, marafiki na familia.

•Dorothy aliolewa mara moja mwaka wa 1965 katika sherehe ya haraka ya mahakama na baadaye alipewa talaka baada ya miaka tisa ya ndoa.

Pete
Pete
Image: SERENDIPITY DIAMONDS

Mwanamke mkongwe kutoka Ohio, Marekani amewashangaza wengi baada ya kujivisha pete ya ndoa mwenyewe katika harusi ya ajabu.

Dorothy Fedeli almaarufu Dottie, 77, ambaye ni mkazi wa O'Bannon Terrace Retirement Home alijioa mwenyewe siku ya Jumamosi katika harusi ndogo iliyoshuhudiwa na majirani, marafiki na familia.

Alisema kuwa hafla ya Jumamosi ilikuwa muhimu sana kwani siku zote alitaka kuwa na ndoa yenye furaha.

"Nilisema, unajua nini, nimefanya kila kitu kingine. Kwa nini isiwe hivyo? Nitajioa mwenyewe," aliwaambia waandishi wa habari.

Mama huyo wa watatu na nyanya wa watoto kadhaa aliolewa mara moja mwaka wa 1965 katika sherehe ya haraka ya mahakama na baadaye alipewa talaka baada ya miaka tisa ya ndoa.

Msimamizi wa mali katika nyumba yake ya ustaafuni, Bw Rob Geiger alisimamia harusi hiyo ya mfano wake huku wageni wakitazama na kusherehekea.

"Ni mwanamke wa ajabu sana na amejaa maisha. Daima amekuwa akiwafikiria wengine,” Rob aliambia TODAY.com.

Kabla ya sherehe hiyo, Fideli alisema kwamba alikuwa na "woga" lakini "alifurahishwa" na siku hiyo kuu. Alifichua kwamba alipata wazo hilo kutoka kwa jirani ambaye alimwona mwanamke akifanya vivyo hivyo kwenye kipindi cha mazungumzo.

Binti yake, Donna Pennington, alimsaidia kupata mavazi, kupika chakula kwa ajili ya tukio hilo na hata kupamba chumba cha wakazi wengine wa nyumba ya wastaafu kwa upinde wa puto na vitu vingine.

"Nilimwambia binti yangu, Hili ndilo jambo bora zaidi ambalo nimewahi kuwa nalo, nje ya kuwa na nyinyi watoto. Hili ndilo jambo ambalo nimekuwa nikitaka siku zote na nina furaha sana kwamba mmenipa," alisema.

"Upendo, upendo ndio kitu muhimu zaidi katika ulimwengu huu, na ukimpenda Mungu na kujipenda, ulimwengu huu utakuwa shamba la maua ya waridi," anasema Fideli.

Fidelli aliwatia moyo wengine wanaojiuliza ikiwa jambo nzuri l itawahi kutokea kwao kwamba kutakuwa na kitu ambacho kitawafurahisha na kuwafanya wajikute maishani na kutimiza roho zao.