(+Video) Jamaa achangisha pesa za mafuta ya Ambulensi baada ya ajali

Watu wameeleza kukerwa kwao na tukio la ambulensi kukosa mafuta.

Muhtasari

•Kijana mmoja alichangisha pesa za kuweka mafuta kwenye gari la wagonjwa ili kuliwezesha kusafirisha majeruhi wa ajali ya barabarani waliokuwa mahututi.

 • Wakaazi walighahabishwa na kitendo hicho huku wakiwashtumu wahudumu wa ambulensi kwa kutowajibika.

Kijana mmoja nchini Ghana alijitwika jukumu la kuchangisha pesa za kuweka mafuta kwenye gari la wagonjwa ili kuliwezesha kusafirisha majeruhi wa ajali ya barabarani waliokuwa mahututi.

Katika video iliyofikia Radio Jambo, kijana huyo alionekana akiwaomba na kuwahamasisha raia waliokuwa wamejumuika kwenye eneo la tukio la ajali kutoa pesa za kujaza tenki ya mafuta ya  Ambulensi hiyo.

Ajali ilitokea wakati gari lililokuwa limebeba nyanya lilianguka na kubingirika. Dereva wa gari hilo aliachwa na majeruhi mengi. Ambulensi lilifika kuwachukua majeruhi lakini la kuhuzunisha ni kuwa gari hilo halikuwa na mafuta na halingeweza kusonga wala kunguruma.

Gari hilo la wagonjwa lilisababisha msongomano mkubwa barabarani huku likishindwa kusonga mbele. Wengi wa waliotazama video hiyo wameeleza kukerwa kwao na suala la ambulensi kukosa mafuta.

Katika video hiyo, wakaazi walighahabishwa na kitendo hicho huku wakiwashtumu wahudumu wa ambulensi kwa kutowajibika.

Kwenye mitandaoni ya kijamii, wanamitandao walieleza kero yao kutokana na kitendo suala hilo. Baahi yao walisema.

''Nimekuja kuhoji nani mwenye mkosa? yaani dereva wa ambulensi alikaa kwenye gari bila kujua kama lina mafuta ya kutosha.'' owoahene alisema.

''Kivipi lakini? Ambulensi bila mafuta. Inasikitisha?'' Beautiful thelma aliuliza.

"Sasa wanachangia pesa kununua mafuta. Kwa kweli ni aibu kwenye nchi kama  hii."  Royaldiva22 alisema.

"Na wabunge wanaendesha magari makubwa ya kifahari na hawakosi mafuta. Ninaipenda nchi yangu, lakini siwezi kuishi hivyo. Huduma za afya zinakasoro." tony_hendrix alisema.

" Kwahiyo Ambulance ilikwenda huko bila mafuta nadhani sio kosa la serikali siku zote ila sisi wananchi lazima tuamke, unawezaje kuendesha gari la wagonjwa bila mafuta?" Dadaeffah aliandika.