14 wathibitishwa kufariki katika ajali iliyohusisha basi la Chuo Kikuu cha Pwani

Wanafunzi na walimu kadhaa wanahofia kuaga dunia.

Muhtasari

•Basi hilo ambalo lilikuwa limebeba zaidi ya watu 30 linaripotiwa kugongana na matatu katika eneo la Kayole, Naivasha.

•Inaripotiwa kwamba basi hilo lilikuwa linaelekea mjini Eldoret kwa hafla ya michezo.

limehusika katika ajali Naivasha
Basi la Pwani University limehusika katika ajali Naivasha
Image: GEORGE MURAGE

Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha yao baada ya basi la chuo kikuu cha Pwani kuhusika katika ajali baya ya barabarani siku ya Ijumaa.

Basi hilo ambalo lilikuwa limebeba zaidi ya watu 30 linaripotiwa kugongana na matatu Alhamisi mwendo wa alasiri katika eneo la Kayole, kaunti ndogo ya Naivasha kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nakuru.

Watu kadhaa walionusurika na majeraha wamepelekwa katika vituo vya afya vya karibu kwa matibabu ya haraka.

Inaripotiwa kwamba basi hilo lilikuwa linaelekea mjini Eldoret kwa hafla ya michezo.

Shughuli za uokoaji zinazoongozwa na polisi na maafisa wakikosi cha zima moto cha Naivasha, kwa usaidizi wa wananchi zinaendelea.

Mkuu wa polisi wa Bonde la Ufa, Tom Odera alisema watu 12 walifariki papo hapo na anahofia huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

“Basi lilibingiria na kuwaua 12 papo hapo. Huenda tukawa na majeruhi zaidi,” alisema.

Alifichua kuwa basi hilo lilikuwa na takriban watu 30—walimu na wanafunzi waliokuwa wakielekea kwenye mashindano ya michezo kabla ya tukio hilo la kusikitisha kutokea.

Odera alisema dereva wa basi hilo alipoteza mwelekeo na kugonga takriban magari matano kabla ya kubingiria kwenye mtaro.