Rwanda imeishinisha kilimo cha bangi ili kuiuza katokasoko la kigheni lakini itsalia kupigwa marufuku nchini humo .
Uamuzi huo wa serikali huenda ukazua utata ikizingatiwa kwamba serikali ya Rwanda ina msimamo mkali sana kuhusu utumizi wa dawa za kulevya huku waraibu wa dawa za kulevya wakikamatwa kila siku na hasa wa bangi
Siku ya jumatatu ambapo uamuzi huo ulitolewa wanawake watatu walikamatwa kwa kuuza bangi .Maamlaka zinasema wanashukiwa kuwa walanguzi wa dawa za kulevya katika wilaya ya Rubavu baada ya kukamatwa na misokoto 1800 ya bangi .
Waziri wa Afya nchini humo Daniel Ngamije amesema licha ya idhini hiyo kwa ajili ya soko la nje ,bangi itasalia haramu nchini Rwanda kwa mujibu wa sheria a taifa hilo .
Mkutano wa baraza la mawaziri ulioongozwa na rais Paul Kagame siku ya jumatatu uliidhinisha mwongozo kuhusu upanzi ,utayarishaji na uuzaji wa bangi .
Kwa mujibu wa sheria nchini humo idhini ya kupanda ,kusambaza bangi itatolewa tu kwa minajili ya matumizi ya matibabu au utafiti .
Haijajulikana jinsi Rwanda itakavyothibti biashara hiyo nchini humo kwani wataalam wamesema utumizi wa bangi umekuwa tatizi la siku huku watu kadhaa wakikamatwa kila siku