- Mataifa mengine yamerejesha masharti makali
- Wengi wamehofishwa na ongezko la visa vya maambukizi
- Kagwe amesema janga litazuka endapo hatua haitachukuliwa
Serikali imezua hofu kuhusu ongezeko la idadi ya visa vya covid 19 nchini.
Kupitia wizara ya afya ,serikali imesema ongezeko hilo limesababishwa na ukiukaji wa kanuni zote zilizowekwa kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo .
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kwa mfano baa haziwahitaji wateja wazo kuvalia maski au kutokaribiana .
Kagwe amesema mikusanyiko ya watu katika mazishi ,harusi na mikutanoo ya kisiasa imerejelewa huku kanuni zote zilizotolewa zikipuuzwa na wahusika .
Hadi kufikia sasa Kenya imesajili visa 44,881 vya Covid-19 huku watu 685 wakipatikana na ugonjwa huo siku ya jumapili .
" Tunahitaji kuangazia takwimu hizi na hasa ongezeko la visa vya wanaoambukizwa na vifo vinavyoripotiwa . Iwapo hazimaanishi lolote basi wajalini wapendwa wenu ..ni jukumu lenu kuwalinda’ amesema Kagwe .
Kagwe amesema wakati rais Uhuru Kenyatta alipolegeza masharti hayo kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 4 lakini sasa kimezidi hadi asilimia 12 .
" Tunaweza kutabiri patatokea janga iwapo hatutachukua hatua za haraka ili kuzuia hili tunaweza kuchagua kati ya kuzama ama kuogelea’ amesema Kagwe
Kulingana na waziri Kagwe watu katika umri wa kati ya miaka 20-39 ndio wanaosheheni asilimia 54 ya visa vyote vya corona .
" Idadi kubwa ya walioaga dunia ni watu walio Zaidi ya umri wa miaka 58 lakini pia tumewapoteza watu walio na umri wa miaka 20 na 30 na leo wazazi wao wanalilia katika makaburi yao’ amesema