Kingi Mashakani

Mahakama yatoa waranti ya kukamatwa kwa gavana wa Kilifi Kingi

Waranti yatolewa kukamatwa kwa gavana wa Kilifi

Muhtasari
  •  Watu wanne  hao  ni  George Ngugi, Abdul Aziz Alim, Moses Musee Maluki  na Noah Akala Aduwo.
  • Hakimu mkuu Eunice Nyutu ndiye aliyetoa waranti hiyo 
Gavana wa Kilifi Amason Kingi

Mahakama moja jijini Nairobi imetoa waranti ya kukamatwa kwa gavana wa Kilifi Amason Kingi  kwa kukosa kuhudhuria kikao cha korti .

Kingi  alifaa kutoa ushahidi katika kesi ya uhalifu ambapo wafanyibiashara wane  wameshtakiwa kwa kujaribu kumlaghai shilingi milioni 30 .

 Hakimu mkuu Eunice Nyutu wa mahakama ya kupambana na ufisadi ya Milimani   pia ametoa waranti ya kukamatwa kwa   Ahemed Ibrahim,  shahidi wa upande wa mashtaka aliyekosa kwenda kortini  .Wawili hao wanafaa kukamatwa na kufikishwa kortini kwa maelekezo zaidi .

 Wakati kesi hiyo ilipofika kwenye ratiba ili kutajwa ,mwendesha mashtaka wa serikali alitaka waranti ya kukamatwa kwao itole2we kwa sababu hawaku mahakamani ili kutoa ushahidi wao .

 Watu wanne wanaoshtumiwa kwa jaribio la kumlaghai Kingi ni  George Ngugi, Abdul Aziz Alim, Moses Musee Maluki  na Noah Akala Aduwo.

 Wane hao ambao ni wafanyibiashara mjini Mombasa  wamekanusha mashtaka dhidi yao .

 Wanadai kujitambulisha kwa Kingi kama maafisa kutoka tume  ya EACC na kwamba walikuwa wakichunguza kesi ya ufisadi dhidi ya Gavana Kingi .