Rais apiga kambi Kisumu

Uhuru awaacha hoi wakaazi wa Kisumu kwa kutua bandarini badala ya uwanja wa ndege wa Kisumu

wakaazi walimtarajia kutua Uwanja wa ndege

Muhtasari
  •  Atazuru miradi mbali mbali inayoendelea katika kaunti hiyo
  • Amekuwa Kisii kupokea ripoti ya BBI 

Rasi uhuru Kenyatta siku ya jumatano  alitua kwa ghafla katika bandari inayokarabatiwa kwa kima cha shilingi bilioni 3 ya Kisumu .

 Rais alitarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Kisumu ambako wakaazi walikuwa wamemngoja huku wapiga ngoma na wanadensi wakitarajia kumlaki .

 Hata hivyo ndege yake ilionekana ikitua katika banadari ya Kisumu na kuwaacha na mafadhaiko wakaazi waliopiga foleni kando ya barabara ya Obote  na ile ya Oginga Odinga ili kumpokea

Uhuru  baadaye alielekea katika Ikulu ndogo  ya Kisumu . Rais alikaribishwa na  kiongozi wa ODM Raila Odinga  ,gavana wa Kisumu  Anyang Nyong'o,  naibu wake  Matthews Owili  na viongozi wengine waliochaguliwa .

 Siku ya alhamisi  Uhuru atakagua  ujenzi unaoendelea wa shilingi bilioni 1.4 wa uwanja wa michezo wa  Jomo Kenyatta International Stadium huko  Mamboleo kisumu mashariki .

 Pia atazuru  eneo la kibiashara Uhuru Business Park linalojengwa kwa kima cha shilingi milioni 350 na  kituo cha kustarehe cha  Jaramogi Oginga Odinga