- Picha ya Amber akiwa amebeba kuku wawili yamtia mashakani
- Amejitetea lakini wengi hawamuamini
View this post on InstagramKumbe ukiacha kujali unaacha kuumia 🤣 #Amberthebrand Outfit @elan_lit
A post shared by Amber Ray 🇰🇪 (@iam_amberay) on
Faith Makau aayejulikana kwa mashabiki wake kama Amber Ray amejipata katika ndimi za wengi hivi karibuni hasa baada ya mpenzi wake wa zamani Brown Mauzo kuanza mahusiano ya kimapenzi na Vera Sidika
Lakini licha ya juhudi zake kujaribu kuendelea na maisha yake bila kufuatiliwa mama huyo wa mtoto mmoja amejipata tena pabaya huku ikitolewa picha moja inayomuonyesha akiwa ‘kwa mganga’ .
Madai kama hayo sio mageni dhidi yake kwani wakati mmoja alidaiwa kujihusisha na mambo ya ushirikina wakati mke mwenza wake wa zamani Aaliyah Zaheer, alipoolewa na mfanyibiashara na mwanasiasa wa Kenya Zaheer Jhanda.
Mwanasosholaiti huyo aliolewa kama mke wa pili wa mwanasiasa huyo wa Kisii Zaheer kwa miaka mitatu na wana mtoto wa kiume ,Gavin .
Wakenya walimhoji kuhusu alichokuwa akifanya baada ya picha hiyo kumuonyesha akiwa amewashika kuku wawili na kufunikwa kitambaa .
Lakini Amber alipata ujasiri wa kuyajibu maswali hayo wakati shabiki mmoja alipotaka kujua mbona anatumia mambo ya ushirika .Faith alimuambia kwamba yeye katu hajawahi kushiriki mambo hayo
Wengi hawakuridhika na jibu lake na akasema kwamba atapata muda baadaye kusema upand wake wa kisa wakati mashabiki watakapokuwa tayari kumuamini .