Alishtakiwa kuendesha kliniki bola kibali

Daktari bandia Mugo wa Wairimu ahukumiwa kifungo cha miaka 3 jela

Alidaiwa kuwabaka wanawake baada ya kuwadunga dawa za kulevya

Muhtasari
  •  
  •  Mugo sio mgeni wa sakata kama hizo 
  • Ni mara ya pili anakabiliwa na mashtaka  hayo 

 

Daktari bandia Mugo wa Wairimu

 

 Daktari bandia Mugo  Wa wairimu amepigwa faini ya shilingi milioni 1.4 na  endapo atakosa kulipa faini huyo atalazimika kuhudumia kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuendesha kituo cha afya bila leseni .

 Katika uamuzi wake uliotolewa siku ya jumatano hakimu mkuu mkaazi Martha  Nanzushi  amesema upande wa mashtaka umethibitisha kesi yake dhidi ya Mugo . pia alishtakiwa kwa kuendesha maabara bila  leseni kutoka kwa   baraza la wahudumu wa maabara nchini

Wairimu  pia alipatikana na hatia ya kuhudumu kama daktari bila leseni .mwaka wa 2018 Wairimu alikanusha mashtaka ya kuendesha kituo cha afya bila leseni na kuhudumu kama muuguzi bila leseni  kutoka kwa maamlaka husika .

Daktari bandia Mugo wa Wairimu

 Muungano wa wauguzi ulijitenga naye ni mara ya pili kwake kutekeleza kosa hilo baada ya kuendesha klini yake mtaani Kayole .

  Katibu mkuu wa muungano wa kitaifa wa waugizi Seth panyako amesema Wairimu hayumo katika sajili ya wanachama wao .

Wairimu, alirejea katika vichwa vya habari  miaka michache baada ya kumdunga mwanamke mmoja dawa ya kulevya na kisha kumbaka  katika kliniki yake isiokuwa na kibali katika mta wa Githurai 44 akihudumu kama mwanajinakolojia