Gharama ya Amani

IEBC: Kura ya maoni ya BBI kugharimu shilingi bilioni 14

IEBC yasema iko tayari

Muhtasari

 

  •  IEBC  imesema iko tayari kwa kura ya maoni 
  •  Tayari zimezuka pingamizi kuhusu mapendekezo ya BBI 

 

Naibu afisa mkuu mtendaji wa IEBC Hussein Marjan

 

Kura  ya maoni kuhusu BBI itawagharimu wakenya shilingi bilioni 14

 Naibu afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo  Hussein Marjan amesema  tayari IEBC  imetengeza orodha ya mahitaji yake ili kufanikisha kura hiyo ya maoni .

" Tumeshaketi chini  na kujiuliza kuhusu yote tunayohitji .Itagharimu shilingi bilioni 14 kuandaa kura hiy’ amesema Marjan

 Amesema wamewazingatia wapiga kura milioni 19.6 na huenda idadi hiyo imeongezeka kwa sababu ya  kuendelea kwa mpango wa kuwasajili wapiga kura .

Marjan  ameyasema hayo alipofika mbele ya kamati ya  bunge kuhusu   uhasibu inayoongozwa na mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi

 Ripoti  ya BBI ilizinduliwa siku ya jumatatu huku mgawanyiko ukiibuka miongoni mwa viongozi wa kisiasa kuhusu baadhi ya mapendekezo yake . Naibu wa rais William Ruto amesimama kidete kupinga baadhi ya   mapendekezo hayo akisema yanafaa kujadiliwa kwa muda Zaidi lakini wanaunga mkono ripoti hiyo hawataki kutumiwa kwa muda Zaidi wa kuijadili au kuifanyia marekebisho wakati huu .