Kikao cha Covid 19

Uhuru aitisha mkutano huku visa vya Covid 19 vikiongezeka

Mkutano utafanyika Novemba tarehe 4

Muhtasari

 

  •  Serikali imehofishwa na ongezeko la visa vya maambukizi 
  • Wakenya wengi wamerejelea shughuli za kawaida huku wakipuuza kanuni zote za kuzuia maambukizi 

 

 

 Rais Uhuru Kenyatta ameitisha kikao kingine kuhusu corona  kati ya serikali kuu na zile za kaunti  kujadili ongezeko la visa vya maambukizi ya corona

 Kupitia taarifa  ta msemaji wa IKULU  Kanze Dena  ,mkutano huo utaandaliwa tarehe 4 mwezi Novemba .

" Kikao hicho  kimeitishwa kwa ajili ya kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya corona  kote nchini  ikizingatiwa kwambakenya ilisajili idadi ya juu ya maafa mwezi oktoba mwaka huu kutokana na ugonjwa wa corona’ imesema taarifa hiyo

 Uhuru amewashauri wakenya kufuata kanuni zilizotolewa na serikali kupitia wizara ya afya ili kuzuia usambaaji wa virusi hivyo .

" wakenya wanafaa kuendelea kuvalia maski  kwa njia ifaayo wakiwa katika sehemu za umma  na kudumisha hali ya usafi wakato wote  kando na kuepuka maeneo yenye mrundiko wa watu’ taarifa hiyo imesema