Uchaguzi wa Tanzania, Tundu ataka Jumuiya za Kimataifa ziingilie kati uchaguzi

Muhtasari

• Tundu ataka Jumuiya za Kimataifa ziingilie kati uchaguzi

• Lissu amedai kuwa mawakala wengi wa upinzania hawakupewa barua ya kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.

Tundu Lissu akihutubia wanahabari siku ya Alhamis. Picha;HISANI
Tundu Lissu akihutubia wanahabari siku ya Alhamis. Picha;HISANI

Mgombea urais wa chama cha upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu ameapa kutokubali matokeo ya uchaguzi mkuu nchini humo kutokana na madai ya udanyifu.

Tundu Lissu amezitaka Jumuiya za kimataifa pamoja na jumuiya za kikanda ziingilie kati taarifa za matokeo ya uchaguzi wa Tanzania.

"EAC, SADC wasitoe taarifa za kuhalalisha uharamia huu. Waseme ukweli. Watanzania waingilie kudai haki yao kwa amani kwa njia ya kidemokrasia,"Tundu Lissu alisema hayo siku ya Alhamisi  katika mkutano na waandishi wa habari.

Aidha ameongeza kusema kuwa chama chake kimeweka wagombea 244 wa ubunge nchi nzima, kati ya hao 63 walienguliwa, udiwani 3754 kati yao wagombea 1025 walienguliwa, hivyo takribani 30% walienguliwa- 'haijawahi kutokea tangu tumefanya uchaguzi wa vyama vingi nchini".

Aliongeza kusema kuwa mbali na kuwa kulikua na changamoto ya kutokuwa na fedha, hawakuweka picha za mgombea nchi nzima lakini "watanzania walituunga mkono".

Lissu amedai kuwa mawakala wengi wa upinzania hawakupewa barua ya kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.

"Mawakala waliobaki kwenye vituo hakuna aliyepewa nakala ya matokeo ya uchaguzi kama sheria inavyotaka,hiyo peke yake inathibitisha hakuna uchaguzi wa vyama vingi, hata kwa sheria zetu kama zilivyo huu haukua uchaguzi majimbo yote , kata zote CCM wametangaza ushindi,"Lissu alifafanua.

Hata hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania imekanusha madai hayo ya upinzani na kusema tuhuma zinazotolewa hazijawasilishwa rasmi.

BBC