Covid 19

Magavana waitisha masharti makali kukabailiana na virusi vya corona

Baraza la magavana lasema kaunti zimeshindwa kuwachukua wagonjwa zaidi

Muhtasari

 

  •  Serikali yashauriwa kurejesha masharti makali  kuzuia maambukizi ya corona 
  •  Magavana wanataka wasiovalia maski kunyimwa huduma katika kaunti 
  • Oparanya asema utekelezaji wa kanuni hizo ndio changamoto kubwa 

 

Mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya   amesema maambukizi ya covid 19 yamekithiri  huku akisema imekuwa vigumu kuwahamisha wagonjwa kutoka kaunti moja hadi nyingine .

 Akizungumza wakati wa kongamano la sita kuhusu  corona kati ya serikali kuu na za kaunti katika Ikulu ya Nairobi Oparanya amesema amesema panafaa kurejeshwa masharti yote ya kupambana na ugonjwa huo.

Oparanya  amesema kumekuwa na utepetevu katika kutekeleza kanuni hizo  hasa katika maeneo ya burudani ,sekta ya uchukuzi na masoko .

" Viongozi wa kisiasa wamekuwa wasambazaji wakubwa wa virusi hivi . Hatua hiyo imesababisha kuongezeka kwa visa vya mambukizi na kufeli kwa juhudi za kuwapata wote waliotangamana na watu walioambukizwa’ Oparanya amesema

 Mwenyekiti huyo wa baraza la magavana alimtaka rais kurejesha muda wa kafyu kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi alfajiri  kwa angalau mwezi mmoja kutoka kipindi cha sasa cha saa tano usiku hadi saa  kumi na moja .

 Serikali za kaunti zitaanzisha kampeini ya  #NoMaskNoService ambapo wasiokuwa na barakoa hawatopewa huduma katika kaunti ili kuhakikisha kwamna wananchi wanavalia maski ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huo

 Oparanya amesema kuongezeka kwa visa vya maambukizi kumefanya vigumu kwa kaunti kuwalaza wagonjwa Zaidi .

" Kwa kweli ni mgogoro mkubwa .wagonjwa wengi wanapoteza maisha yao wakisafirishwa kwenda Nairobi  ili kupata matibabu’ amesema

 Ameongeza kwamba kaunti 12  hazina vitanda 300 kama inavyohitajika ilhali kaunti 11  vina chini ya vitanda 5 vya ICU.` Kuna uwezekano wa rais Uhuru Kenyatta kufunga baadhi ya sehemu za nchi  au kuongeza muda wa kafyu wakati  atakapokutana na baraza la usalama wa kitaifa baadaye wiki hii