Uteuzi

DPP Haji awateua tena Taib, Kihara kama waendesha mashtaka wa serikali

Watahudumu kwa miaka 2 zaidi

Muhtasari
  • DPP awateua mawakili wawili a hadhi ya juu kwa miaka 2 zaidi 
  •  Taib na Kihara walihusika katika uchunguzi dhidi ya naibu jaji mkuu Philomea Mwilu 

 

Taib Ali Taib

Mkurugenzi wa mashtaka ya umm Noordin Haji amewateua  Taib Ali Taib na James Kihara kama waendesha mashtaka wa serikali kwa miaka miwili Zaidi

Kupitia arifa ya gazeti rasmi la serikali  Taib  na Kihara watahudumu kuanzia januari  tarehe 16 mwaka wa 2021 kwa miaka miwili .

" ... Baada ya kuhitimu kama mawakili wa serikali kwa miaka miwili Zaidi’ arifa hiyo imesema

 Mawakili hao wawili wataisaidia afisi ya Haji  kukabiliana  uhalifu nchini tangu waanzishe jukumu la kupambana na visa vya ufisadi mwaka wa 2018 .

 Kundi hilo lilikuwa sehemu ya mawakili waliosaidia katika uchunguzi  wa madai ya ufisdi dhidi ya naibu jaji mkuu Philomena Mwilu