- Chelugui amesema hazina hiyo itawasaidia wasio na ajira na wanaopoteza kazi zao
- ILO imesema watu milioni 26 watakosa kazi kote duniani kwa ajili ya janga la corona
Serikali ya kitaifa inapanga kuzindua hazina maalum ya kuwasaidia wafanyikazi wanaopoteza kazi zao .
Waziri wa Leba Simon Chelugui amesema hazina hiyo itakuwa sehemu ya mpango wa kukwamua uchumi kutoka kwa makali ya janga la corona . Amesema licha ya mwongozo wa kupambana na corona kupunguza idadi ya maambukizi ,kanuni hizo pia zimesababisha watu wengi kupoteza kazi zao .
Chelugui amesema serikali itafanya tathmini ya athari ya janga la corona kwa wafanyikazi wahamiaji .
Biashara nyingi kote duniani na hasa zile ndogo ndogo na za kadri zimesajili hasara kubwa na nyingine kulazimika kufungwa .
Sekta ya jua kali nchini Kenya amayo huwajiri asilimia 59.9 ya wafanyikazi imeshuhudia idadi kubwa ya watu waliopoteza kazi zao .
Huduma za kijamii na kibinafasi kama vile saluni na vinyozi pia zimeathiriwa – amesema Chelugui .
Machi mwaka huu shirika la kimataifa la leba ILO lilisema kwamba janga la corona litasababisha watu milioni 25 kote duniani kukosa ajira .